Wafanyakazi zaidi ya 50 wa hoteli ya Kitalii ya Ngurdoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha ,wameandamana ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakimlalamkia mwajiri wao Joan Mrema kwa kushindwa kuwalipa mishahara yao ya miezi mitatu mfululizo.
Wakiongea mbele ya Mkuu huyo wa wilaya wamedai kuwa pamoja na kutolipwa mishahara yao ,wanadai makato ya mfuko wa kijamii wa nssf yamekuwa hayapelekwi na kupatĂ usumbufu mkubwa wanapoacha ama kuachishwa kazi .
Madai mengine ni wafanyakazi wa kike wa hoteli hiyo pindi wanapokuwa kwenye likizo ya uzazi (Maternity Leave) mishahara yao husitishwa hadi atakaporejea kazini.
Baadhi ya wafanyakazi hao Yona Estomi,Stela Shayo na Dominy Kwayu wamedai kwamba kuanzia mwaka Jana mwezi wa 12 hawajalipwa mishahara yao na kusababisha hali ya maisha kuwa ngumu na baadhi yao kufukuzwa kwenye nyumba wanazopanga wanazoishi.
"Hivi sasa unapotuona hapa baadhi yetu tumefukuzwa kwenye nyumba tunazoishi na watoto wetu wamerudishwa shule tunadai mishahara ya miezi mitatu hatuelewi tutalipwa lini tunaomba serikali itusaidie tuweze kulipwa " Amesema Shayo.
Naye mfanyakazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Matata alisema kuwa,amefanya kazi kwa muda wa miaka 17 sasa kama kibarua na hajawahi kuajiriwa ,ambapo alipojaribu kudai fedha zake alifukuzwa kazi na haelewi cha kufanya,hivyo anaomba Mkuu wa wilaya hiyo aweze kuwasaidia ili wapate hali zao .
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro baada ya kuwasikiliza wafanyakazi alisema amepokea malalamiko ya wafanyakazi hao na kuahidi kutatua suala hilo ikiwemo kuwakutanisha na mwajiri wao ambaye aje kueleza kwann hataki kulipa mishahara ya wafanyakazi.
"Nimewasikiliza vya kutosha kinachofuata ni kuwakutanisha na mwajiri wenu unajua huyu ni mwekezaji mzawa lazima tumlinde ili kuhakikisha analipa malipo yote ya serikali ikiwemo mishahara yenu"
"Mimi kama Mkuu wa wilaya yenu nimeyachukua malalamiko yenu na kuanza kuyashughulikia muwe wavumilivu ndani ya wiki moja tunamaliza suala lenu"Amesema Muro.
Kwa upande wake meneja wa hoteli hiyo baada ya kupigiwa simu na DC Murro,Beatrice Dallas aliomba apewe wiki moja aweze kushughulikia suala la malipo ya wafanyakazi kwa sababu hali ya kibiashara ni mbaya sana.
" Mheshimiwa tunaomba wiki moja utupatie tuweze kushughulikia malipo ya wafanyakazi maana hali ya kibiashara ni mbaya sana najua wanatudai ila lazima watupe muda"Amesema Beatrice.
Hata hivyo DC Muro amemtaka meneja huyo kufika ofisini kwake kesho Ijumaa Machi 6/2020 SAA tano, asubuhi ili kujibu kwanini wameshindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...