Na Karama  Kenyunko

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia, William  Ole Nasha  amesema wako mbioni kuhuwisha sera ya teknolojia ili kuwezesha usimamizi wa kazi za ubunifu na kuongeza  udhibiti kwenye kazi hizo.

Akizindua wiki ya ubunifu  iliyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF), Ole Nasha amesema serikali ya awamu ya tano inaangalia kwa ukaribu teknolojia na mawazo yenye tija yanayobuniwa kwa lengo la kufanikisha lengo la kuwa  uchumi wa viwanda.

Alisema Tanzania ya viwanda haiwezi kufanikiwa kama hakuna wabunifu, ndiyo maana wako makini ili kuhakikisha wanapata mawazo mapya na yenye tija.

“Nafarijika kuona vijana wa Kitanzania wanaumiza vichwa  kubuni mawazo na teknolojia ambazo zina manufaa makubwa katika kutatua changamoto katika jamii hivyo, vijana hasa wa maeneo ya vijijini  sehemu ya utatuzi wa changamoto zilizopo kwenye jamii kubuni teknolojia," amesema Ole Nasha.


Ameeleza kuwa  serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha bunifu zenye tija zinatumika kibiashara na kuleta manufaa kwa wabunifu.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa ubunifu wa maendeleo ya binadamu (HDIF) Joseph Manirakiza amesema ni wakati sasa kwa wabunifu kuanza kufikiria utatuzi wa changamoto zilizopo katika jamii.

“Tunaposema buni kwa tija ina maana yanahitajika yale mawazo yanayotatua changamoto tulizonazo. Kama hatuna wabunifu basi tutaendelea kubaki kama tulivyo,”


 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William  Ole Nasha akizungumza na wadau wa maendeleo na wabunifu wakati akizindua Wiki ya Ubunifu 2020 leo jijini Dar es Salaam ambayo inakutanisha zaidi ya wadau na wabunifu 6,000
 Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi  na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu  akizungumza wakati wa uzinduzi  wa Wiki ya Ubunifu  2020 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...