USAJILI kwa wajasiliamali wadogo wanaotumia kemikali katika kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa sasa ni shilingi elfu kumi kwa kemikali moja kwani serikali inabeba majukumu la kila mjasiliamali mdogo hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko wakati akifunga mafunzo kwa wajasiliamali wadogo jijini Dar es Salaam leo huku akitoa vyeti kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo juu matumizi sahihi ya kemikali wanazotumia kutengeneza bidhaa mbalimbali.

"Kwa kila kemikali kwa hili kundi usajili utakuwa shilingi elfu kumi, kwani maswasiliano kati yenu na serikali nayanafanya serikali kubeba mzigo huu, kwa kutambua mchango wa wajasiliamali wadogo." 

"Kemikali mnazotumia zikichepushwa kwenye matumizi yake halali zinaweza kutengeneza kitu kingine chenye madhara kwa afya ya binadamu." Amesema Dkt. Mafumiko.

Amesema kuwa ili kuhakikisha matumizi salama ya kemikali kuwa ni salama Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa sheria kila mdau anayejishughulisha iwe kwa kuuza, kutumia kemikali hizo, iwe kwa kuingiza kutoka nje ya nchi au kutoa nje ya nchi ama kusafirisha kulingana na sheria hiyo inabidi asajiliwe na msajili wa kemikali kutoka Ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali.

"Na mkishasajiliwa,lazima kukamilisha usajili unaambatana na kupata cheti, ambacho kinakuruhusu kufanya shughuli ya kutumia kemikali." Amesema Dkt. Mafumiko.

Licha ya hiyo Dkt. Mafumiko amesema kuwa aina ya kemikali zilizobainishwa na kusimamiwa na sheria hii ni pamoja na zile zote zinazotumika kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo wajasiliamali wengi wanazizalisha bidhaa.

Ninyi ndio tunawategemea kuwa mabalozi kwa wengine ili tupanue wigo wa wajasiliamali kwa manufa yetu sisi na manufaa binafsi kwani kemikali zinazotumika zikitumika vizuri ni kwa manufaa na zikitumika vibaya zinaweza zikaangukia kwenye mikono mibaya na zikatumika kama vilipuzi na kemikali nyingine zinaweza kuleta madhara kwa afya ya binadamu.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiliamali wadogo wakati wa kufunga mafunzo kwa wajasiliamali hao leo jijini Dar es Salaam.
 Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko  akizungumza na wajasiliamali wadogo wakati wa kufunga mafunzo jijini Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wajasiliamali wadogo wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko jijini Dar es Salaam leo.







  Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akitoa vyeti kwa  akiwajasiliamali wadogo wakati wa kufunga mafunzo jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...