Charles James, Michuzi TV

TANZANIA itaungana na Mataifa mengine duniani kuadhimisha wiki ya maji ambayo itaanza Machi 16 hadi 22 mwaka huu huku kauli mbiu ikiwa ni " Maji na mabadiliko ya tabia nchi, uhakika wa maji salama kwa wote".

Wiki ya maji itaenda sambamba na siku ya maji ambapo ndio itakua kilele cha maadhimisho hayo ambayo yalianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1993 kupitia azimio na.47/193 ililofikiwa mwaka 1992 na Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na wandishi wa habari  leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo amesema katika wiki hiyo Tanzania itaungana na Mataifa mengine duniani katika kutathimini mafanikio ya changamoto zilizojitokeza katika sekta ya maji katika kipindi cha miaka mitano.

Prof Kitila amesema wiki hiyo ya maji pia itaenda sambamba na uzinduzi wa miradi ya maji ambayo imekamilika na itaongozwa ba Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wa kiserikali.

" Kwenye wiki ya maji tutakua na mkutano wa kisayansi wa wataalamu wa maji utakaofanyika Machi 17-18 katika ukumbi wa Mikutano wa APC uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam na mkutano huo utafunguliwa na Makamu wa Rais Mhe Mama Samia Suluhu Hassan.

Pia tutakua na mkutano wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira utakaofanyika Machi 19-20 lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto za mamlaka za maji na usafi wa mazingira katika kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, " Amesema Prof Kitila.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo pia utapokea taarifa ya utendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kutoka kwa mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) ambapo taarifa ya tathmini ya utendaji wa mamlaka itazinduliwa na Mhe Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Prof Kitila amesema kutakua na mkutano wa pamoja kati ya serikali na wadau wa sekta ya maji utakaofanyika Machi 21 mwaka huu ambao utakutanisha serikali na washirika wa maendeleo na wadau mbalimbali wanaochangia sekta ya maji.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma kuelekea wiki ya maji duniani.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo akizungumza mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma kuelekea wiki ya Maji itakayoanza Machi 16-22 mwaka huu.
 Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dodoma wakifuatilia mkutano wao na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo ambao ulikua ukizungumzia maadhimisho ya wiki ya Maji itakayoanza Machi 16-22 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...