Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu ya jamii

KAIMU Kamishina Jenerali wa Mamlaka  ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini James Kaji amesema kuwa Tanzania imefanikiwa kupunguza kwa asilimia 90 uingizwaji wa dawa za kulevya nchini kupitia ukanda wa Bahari ya Hindi na kwamba  Serikali ya Awamu ya Tano imepongezwa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la UNODC linaloshughulika na dawa hizo na uhalifu kutokana na kutambua juhudi zake katika kukomesha biashara hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna Jenerali Kaji amewaambia waandishi wa habari  kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti biashara ya dawa za kulevya na vema Watanzania wakaendelalea kushiriki kikamilifu kwenye vita hiyo na hatimaye kupunguza au kumaliza kabisa uingizwaji wa dawa hizo.

" Shirika hilo kupitia Kamisheni ya kimataifa ya kudhibiti Dawa za kulevya (CND )  imeipongeza Tanzania  kwa jitihada madhubuti katika kudhibiti na kupambana na tatizo la dawa za kulevya ambazo zimeleta matokeo chanya katika mapambano ya dawa kulevya duniani kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuazia mwaka 2018 hadi 2020.

Amefafanua kuwa katika mkutano wa 63 wa kamisheni ya kimataifa ya kudhibiti Dawa za kulevya duniani  (CND 63) uliofanyika Viena - Austria ,Mkuu wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na masuala ya dawa kulevya na uhalifu  (UNODC) Ghana Fathi Wally amesema Tanzania ni moja kati ya nchi chache barani Afrika zilizofaikiwa kupunguza upatikanaji  na uhitaji wa dawa za kulevya pamoja na kupunguza madhara yanayosanabishwa na matumizi ya dawa hizo, kuimarishwa ushirikiano wa kimataifa na kuwekeza kutekeleza mikakati minne ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya Kwa uwiano ulio sawa."amesema Kaji

Kaimu Kamishna Jeneral Kaji amesema kuwa mafanikio haya yamekuja kutokana na juhudi za Serikali ya Tanzania kufanya marekebisho makubwa ya kisheria Kwa kutunga sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya sheria Na.5 ya mwaka 2015 na mabadiliko yake ya mwaka 2017 Kwa Tanzania bara,na kwa upande wa Tanzania visiwani ambako mabadiliko ya sheria yamefanyika 2019.

Pia amesema kutokana na mafanikio hayo mwaka 2018 Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya Dawa za kulevya na uhalifu (UNODC) liliipa Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 28 wa umoja wa Mataifa Kwa kanda ya Afrika wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na tatizo la dawa za kulevya (HONLEA 28 ) uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema pamoja na mafanikio hayo makubwa kwa masikitiko makubwa kuna baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania vimekuwa vikiandika na kutoa taarifa za upotoshaji kiasi cha kurudisha nyumba jitihada hizo na mbaya zaidi zinachafua taaswira ya nchi yetu kazi.

Amesisitiza ni muhimu kuwa makini katika uandishi wa habari na ni vema kutumia vyanzo vya uhakika na kuzingatia maadili ya uandishi .Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya kifungu cha 7(2) ina wajibu wa kutoa taarifa sahihi kwa jamii ya watanzania kuhusu masuala ya dawa za kulevya na kwamba kwa vyombo vya habari  kifungu hicho vinawajibu kutoa habari sahihi kwa wananchi kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria.

Pia ameeleza kwamba  Mamlaka hiyo iko wazi na tayari wakati wote kutoa ushirikiano hususani kutoa taarifa za masuala yanayohusu dawa za kulevya nchini huku akifafanua kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti  na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji akisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
 Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji akiwa ameshika gazeti na nakala zenye habari za upotoshaji zinazohusu mamlaka katika jitihada za Kupambana na biashara ya dawa hizo ambapo ametumia nafasi hiyo kuomba vyombo vya habari kuandika habari zenye usahihi badala ya kupotosha
Baadhi ya wakuu wa Idara ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wakifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo James Kaji leo jijini Dar es Salaam
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...