Na Issa Mzee Maelezo Zanzibar 12/03/2020.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali
Mbarouk amesema kuwepo kwa tatizo la umeme mdogo katika baadhi ya maeneo ya mji
wa Zanzibar yanatokana na ongezeko la watumiaji pamoja na ujenzi holela.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake huko Gulioni Mjini Unguja kuhusiana na mafanikio na
changamoto zinazoikabili shirika hilo.
Amesema Shirika hilo linachukua jitihada ya kufunga
mashine kubwa (transfoma) katika maeneo hayo ili kuweza kukidhi mahitaji ya
matumizi na kuondosha usumbufu kwa wananchi.
Meneja huyo amefahamisha kuwa shirika hilo
linakabiliwa na changamoto ya wizi wa mita, umeme, baadhi wananchi na mashirika
kutolipa madeni kwa wakati na utapeli unaofanywa na baadhi watu kujifanya
watumishi wa shirika hilo kwa lengo la kuiba na kupelekea kulitia hasara
shirika.
“Licha ya kuwa shirika linachukua jitihada za
hukakikisha kuwa upatikanaji wa huduma ya umeme mijini na vijijini upo vizuri lakini
bado tunakabiliwa na changamoto ya wizi wa mita, umeme, baadhi ya wananchi na
mashirika kutolipa madeni yao kwa wakat, na matapeli wanaolaghai wananchi kwa
kujifanya watumishi wa shirika kwa lengo la kuibia wananchi jambo ambalo hukosesha
mapato ya shirika”.
Aidha ameeleza kuwa matumizi ya umeme yamepanda kwa
kasi Zanzibar kutoka mega watt 40 mwaka
2008 na kufikia mega watt 70 mpaka 90 mwaka huu ambapo shirika hilo lina uwezo
wa kuzalisha mega watt 140 kwa siku
Akizungumzia mafanikio Meneja huyo amesema shirika
hilo limefanikiwa Meneja huyo alisema
shirika hilo limeweza kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kufikisha
umeme vijijini na katika visiwa vidogo
vya Unguja na Pemba.
“Katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi shirika limeweza kufikisha umeme vijijini na katika visiwa
vidogo vya Unguja na Pemba, ambapo vijiji
520 vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo nane kati ya kumi vilivyotakiwa
kupata umeme tayari visiwa nane vinapata nishati hiyo”, ameeleza Meneja huyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu deni la bilioni 65 linalodaiwa
shirika la umeme la Zanzibar na shirika
umeme Tanzania Bara (TANESCO) amesema kuwa tayari fedha zimeshalipwa ambapo zimebaki bilioni 10.7 kumalizia deni
hilo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk
akizungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu Utendaji Kazi katika Shirika hilo
Huko Ofisini kwake Gulioni Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa habari
Wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali
Mbarouk kuhusu Utendaji wa Kazi katika Shirika hilo hafla iliyofanyika Ofisini
kwake Gulioni Mjini Zanzibar.Picha Na
Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...