Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani
humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao ambayo
ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa
lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
Sita wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita
mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao
ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Afisa Afya wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Reuben Malimi akitoa elimu ya tahadhari dhidi ya Homa ya Mapafu
inayosababishwa na Virusi vya Korona kwa wanafunzi wa kidato cha Sita
mkoani humo waliokuwa katika kambi ya Kitaaluma shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Maswa, kabla ya kambi hiyo kufungwa ili kuchukua tahadhari
dhidi ya Corona.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
Sita wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita
mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao
ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu,
Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya kambi ya kitaaluma kwa
waanfunzi wa kidato cha sita mkoani humo, kabla ya kumkaribisha Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kuzungumza na wanafunzi
hao, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao , ambayo
ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa
lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
……………………………………………………………………………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Uongozi wa Mkoa
wa Simiyu umefunga kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha Sita
mwaka 2020 iliyokuwa ikifanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa , ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Homa kali ya Mapafu
inayosababishwa na Virusi vya Corona.
Akifunga
kambi hiyo, Machi 16, 2020 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini amesema uongozi wa mkoa umefikia hatua hiyo kuchukua tahadhari
kama ilivyoelekezwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa juu ya kuzuia
mikusanyiko ya watu wengi isiyo ya lazima katika kipindi hiki ambacho
kumeripotiwa idadi ya watu kadhaa kubainika kuwa na virusi vya Corona
katika nchi mbalimbali.
“Kutokana na
Maelekezo ya Serikali Mkoa umeona kambi hii ifungwe kwa ajili ya
tahadhari dhidi ya Corona, Mhe. Rais amesitisha mbio za Mwenge wa Uhuru
kwa mwaka 2020, Mhe. Waziri Jafo amesitisha UMISETA na UMITASHUMTA na
tahadhari mbalimbali zimeendelea kutolewa na Serikali ikiwemo ya kuzuia
mikusanyiko; sisi hapa tuna wanafunzi takribani 1000 kutoka shule 10
hivyo tumekubaliana kwa pamoja tuifunge kambi hii,” alisema Sagini.
Aidha, Sagini
amesema pamoja na kambi za kitaaluma kufungwa Mkoa utaendelea kusimamia
utekelezaji wa mkakati wa taaluma wa mkoa ili walimu, wanafunzi na
wadau wengine wa elimu waweze kutimiza wajibu wao kuhakikisha Mkoa
unatimiza adhma yake ya kuwa miongoni mwa mikoa itakayofanya vizuri
katika mitihani yote ya Kitaifa.
Kwa upande
wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema wanafunzi
hao walitakiwa kukaa kambini muda wa wiki sita kwa ajili ya maandalizi
ya Mtihani wa Taifa unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei 2020, hivyo pamoja
na kusitisha kambi hiyo walimu wamehimizwa kutimiza wajibu wao katika
ufundishaji na wanafunzi wametakiwa kwenda kusoma kwa bidii ili kufikia
lengo la Mkoa.
Awali akitoa
elimu ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona
kwa wanafunzi na walimu kabla ya kambi kufungwa, Afisa Afya wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Reuben Malimi amesema ugonjwa huo hauna tiba matibabu
yanayofanyika yanazingatia dalili zinazoonekana kwa mgonjwa, hivyo ni
vema kila mmoja akachukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo na elimu
inayotolewa na wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali.
Nao wanafunzi
wa Kidato cha Sita wa Mkoa wa Simiyu wameshukuru uongozi wa Mkoa
kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwa kutoa elimu kuhusu
Corona kabla ya kufunga kambi, huku wakieleza namna ambavyo kufungwa
kwa kambi kunaweza kuathiri malengo yao waliyojiwekea.
“Tunashukuru
uongozi wa Mkoa kutoa elimu na kuchukua tahadhari ya Corona kwa kufunga
kambi ni hatua ya kutuhakikishia usalama, lakini kambi ilitusaidia
kujua namna ya kujibu maswali ya mtihani wa Taifa na kujifunza mada
ngumu tulizoshindwa shuleni kupitia kwa walimu mahiri, tutatumia muda
huu kujisomea kwa bidii ili tufaulu vizuri mtihani wa Taifa,” alisema
Isack Ndassa kutoka Shule ya Sekondari Kanadi Itilima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...