Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza akifafanua jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa wa Chama cha United Democratic Party (UDP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa UDP Taifa, John Momose Cheyo.
Mkuu wa Idara ya Gharama za Uchaguzi na Ruzuku toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bi. Hollo Kazi akielezea jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa wa
Chama cha Wakulima Tanzania (AAFP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Afisa Mipango wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Emmanuel
Msengi.
Afisa Mipango wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Emmanuel Msengi akifafanua jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa wa Chama cha Wakulima Tanzania (AAFP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Zoezi la uhakiki limeanza leo ambapo jumla ya vyama sita vimehakikiwa ambavyo ni AAFP, ADC, UMD, UDP, NLD na NRA.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AAFP), Bw. Rashid Rai akijibu hoja wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembelewa na Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dar es Salaam. Zoezi la uhakiki limeanza leo ambapo jumla ya vyama sita vimehakikiwa ambavyo ni AAFP, ADC, UMD, UDP, NLD na NRA. Viongozi wa chama cha AAFP wamevaa maski ikiwa ni tahadhari ya kuambukizwa ugonjwa wa Corona Virus.
Mhazini wa Chama cha Wakulima (AAFP), Bw. Ndonge Said Ndonge akitoa maelezo kuhusu namna wanavyo tunza taarifa zao za mapato namatumizi mbele ya Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) walipofika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho kwa ajili ya zoezi la uhakiki lililoanza leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa nje wa Ofisi za Vyama vya siasa vya AAFP na UDP (Na: Mpiga picha wetu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...