Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devota Mayala kulia akitoa ufafanuzi wa huduma za mamlaka hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari wakati alipotembelea banda lao kwenye eneo la viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika eneo hilo.
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga.
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda lao
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeeleza kwamba vitu ambavyo vinasababisha bili za maji kuwa kubwa ni matumizi ya maji na kutokukaguliwa kwa miundombinu iliyopo kwenye nyumba mara kwa mara kama bomba linavuja au limedondokewa na kitu kupasuka na kumwaga maji .
Upasukaji huo wakati mwengine umekuwa hautambuliki mapema na hivyo kupelekea ongezeko la bili kubwa jambo ambalo lingeweza kudhibitiwa iwapo kungekuwa na utaratibu nzuri wa kufanyika ukaguzi huo mara kwa mara kwenye miundombinu hiyo.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devota Mayala wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.
Alisema kwamba walitumia siku hiyo pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zao za maji safi na uondoshaji wa maji taka ambapo katika suala hilo mtumiaji mkubwa ni mwanamke kwa sababu walipaji wa bili ni wakina baba na watumiaji wakubwa ni wakina mama ndio wanatumia kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
“Bili kubwa inasababishwa na vitu vingi ikiwemo matumizi ya maji, miundombinu iliyopo kwenye majumba yetu kama watu hawana utaratibu wa kukagua mabomba unakuta linamwaga maji au limedondokewa na kitu likapasuka bila watu kujua na hivyo maji yakimwagia kwenye mita inaandika maji yametumika”Alisema
Alisema kitu kingine ni hitilafu kwenye mita hali inayochangia uwepo wa bili kubwa ambazo huzielewi huku gharama unazolipa zisizo sahihi unaruhusiwa kufika ofisini na kuonana na wahusika na kuambiwa ufanye nini ili ikiwemo upimaji wa mita yako.
Hata hivyo alisema mita itapimwa na utaonyeshwa kama inashida na baadae itabadilishwa kwa hiyo wapo kwenye maadhimisho hayo kuwaelimisha wakina mama na wananchi kuhusiana na suala hilo.
Awali akizungumza Afisa Utawala wa Tanga Uwasa Theresia Sanga alisema kwamba wataendelea kutoa elimu kuhusiana na uondoshaji maji taka majumbani ikiwemo kuacha kufanya uhujumu wa miundombinu ya maji na maji taka.
Aliwataka wananchi waliounganishwa na mtandao wa maji taka kuutumia vizuri na kutokuweka taka ngumu kwani inaweza kupelekea kutokupitisha maji vizuri.
“Lakini pia nitoe wito kwa wananchi kwenye maeneo ambayo mtandao wa maji taka umepita wateja wajiunge na mtanda huo pamoja na kuacha kuhujumu miundombinu hiyo kwa kutupa taka ngumu kwani wanakuwa wakiihujumu taasisi hiyo kwani wanatumia fedha nyingi kuirejesha kwenye hali yake ya kawaida”Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...