Na Said Mwishehe,Michuzi Blog ya jamii


NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( SADC) zimechukua hatua ya vikao vyake kikiwemo cha Baraza la Mawaziri katika nchi hizo kufanya vikao kwa njia ha Video ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa Corona ( COVID -19 ).

Akizungumza leo Machi 10 mwaka 2020 ,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert Ibuge amesema kuwa hatua hizo zimetokana na ushauri uliotolewa katika mazimio ya kikao cha maziri wa afya wa SADC ,hivyo kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilichopangwa kutanguliwa na kikao cha maofisa waandamizi Machi 12 hadi Machi 14 mwaka huu kimefupishwa na sasa litafanyika kwa njia ya video kuanzia Machi 16 hadi Machi 18 mwaka huu.

"Utaratibu wa mkutano wa baraza la mawaziri unaotarajiwa kufanyika Tanzania kama Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo utabadilika kwa kuufanya mkutano huo kwa njia ya video ambapo mawaziri watakuwa wakifanya mkutano katika nchi zao.Utararibu huo wa kuendesha mkutano kwa njia ya video umeridhiwa na sekretarieti ya SADC pamoja na nchi Mwenyekiti kwa kuwa unalenga kuondoa hatari ya kuenea kwa ugonjwa huo hatari ambao tayari umeshafika katika nchi mwanachama wa SADC ,Afrika Kusini,"amesma Balozi Ibuge.

Aidha amesema Tanzania kama Mwwnyekiti wa SADC inatoa rai kwa Serikali na wananchi wa Jumuiya ya SADC kuchukua hatua stahiki zinazopendekezwa na wataalaam wa afya kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao umeshafika katika nchi mwanachama wa SADC , Afrika Kusini." Utaratibu mpya wa kufanya mkutano kwa njia ya video kwa namna moja au nyingine utaleta athari kwa nchi yetu ambayo Serikali na wananchi wake walishajiandaa na mapokezi ya wageni hao kwa kuwa wafanyabiashara wa hoteli, usafiri,chakula na makundi mengine walishafanya maandalizi."

Balozi Ibuge ameongeza pamoja na athari hizo Serikali inaungana na nchi wanachama wa SADC kuona umuhimu wa kulinda afya za wananchi wake kwa kuepuka mikusanyiko yetote inayohatarisha kuenea kwa ugonjwa huo na kwamba Serikali inatoa shukrani kwa vyombo vya habari kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha katika kuutaarifu Umma kuhusu uteketezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya SASC hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Pia Serikali inatoa mwito kwa vyombo vya habari kuendelea kuhabarisha Umma kuhusu masuala muhimu yakayojadiliwa katika vikao vya baraza la mawaziri wa SADC kitakachofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam na kuongeza Baraza la Mawaziri wa SADC litaendeshwa chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na kushirikisha mawaziri wanaoshughulikia mambo ya nje,viwanda,biashara, fedha na mipango kutoka nchi wanachama wa nchi hizo.

Hata hivyo Balozi Ibuge Ibuge awali kabla ya kuzungumzia uamuzi huo wa mikutano kufanyika kwa njia ya video, alieleza kuwa Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) inaendelea na mandalizi ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopangwa kufanyika Machi 16 na 17 mwaka huu.

Miongoni mwa ajenda muhimu zilizopangwa kujadiliwa katika mkutano wa baraza la mawaziri ni utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka ya Jumuiya hiyo inayosema Mazingira wezeshi kwa ajili ya maendeleo endelevu na jumuishi ya viwanda,kukuza biashara na ajira ndani ya SADC .

Ajenda nyingine ni masuala ya fedha na michango ya Jumuiya,tathimini ya utangamano itakayowezesha nchi wanachama kujipima kuhusu utekelezaji wa malengo ya Jumuiya baada ya 2020-2030 .Ajenda nyingine ni maadhimisho ya miaka 40 ya SADC ,upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia ujumbe wa SADC na uanzishwaji wa Shirika la Utalii kwa nchi wanachama.

"Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kimetanguliwa na kikao cha dharura cha mawaziri wa sekta ya afya kilichojadili hali halisi ya Corona duniani na katika nchi za jumuiya, maandalizi ya nchi za SADC katika kukabiliana na ugonjwa huo pamoja na hatua za kuchukuliwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa kwa nchi zetu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) ambao kwa sasa umeikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari kuhusua Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) ambao kwa sasa umeikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.
Naibu Katibu Mtendaji wa Maswala ya Ushirikiano wa Kikanda (SADC) Thembinkosi Mhlongo akifafanua ajenda ya Mfumo mpya wa Hati ya Kusafiria za SADC itakayojadiliwa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi wanachama wa jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha Uchumi pamoja na viwanda na Biashara,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wapili kutoka kushoto aliyevaa koti rangi Nyeusi) akiwa na wajumbe wengine wa SADC mara baada ya kuwasili katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.Picha na Michuzi JR-Michuzi Media.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...