Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu ya jamii
NCHI ya Ufaransa imesema kwamba imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 1.10 kwa ajili ya kutoa mafunzo ya lugha ya Kifaransa kwa walimu na maprofesa mbalimbali nchini Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha lugha hiyo inazungumzwa na Watanzania wengi.
Kwa mujibu wa Ufaransa ni kwamba mkakati wa nchi hiyo ni kuhakikisha lugha ya Kifaransa inaendelea kuwa na watu wengi zaidi ambao watakuwa wanaizungumza kwa ufasaha na kuitumia kama sehemu muhimu ya Mawasiliano kati ya nchi moja na nyingine zikiwemo nchi zinazozungumza Kifaransa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema kuwa lengo la nchini yake kutenga fedha hizo ni katika muendelezo wa kuona lugha hiyo inatumiwa na Watanzania wengi na njia mojawapo ni kutoa mafunzo kwa walimu na maprofesa ambao hao watakuwa na jukumu la kufundisha lugha hiyo kwa Watanzania wengine.
Akifafanua zaidi kwenye mkutano wa pamoja wa mabolozi wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa ambao wako nchini Tanzania, Balozi Clavier amesisitiza kwamba fedha hizo ni kwa ajili ya mkakati wa mwaka 2020/2021 na baada ya hapo zinaweza kuongezwa kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.
" Tungependa kuona na Tanzania kama ilivyo kwa Morocco, DRC na Comoro nayo inaingia kwenye kundi la nchi zinazozungumza kifaransa (Francphonie)," amesema Balozi Clavier.Pia amesema katika maadhimisho ya miaka 50 ya umoja wa nchi hizo zinazozungumza kifaransa, kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoadhimishwa kwa wiki moja kuanzia Machi 17 mpaka 28.
Amefafanua kuwa Ufaransa inapenda kuona Tanzania kama nchi inaingia kwenye kundi la nchi za Francphonie, hii ni sababu ya kutenge fedha kuendeleza kifaransa hapa Tanzania na wanaamini kuwapa wasomi wakielewa lugha ya Kifaransa kutasaidka kuwafundisha wengine.
Balozi Clavier ameeleza kuwa lugha ya Kiiswahili ni lugha kubwa kama ilivyo Kingereza na Kifaransa, lakini ni wakati muafaka kwa Tanzania nayo wananchi wake kujifunza Kifaransa kama lugha kubwa ya Mawasiliano.
Ufaransa tunayo programu maalum ya udhamini wa masomo ya kifaransa kuanzia hapa nchini na kuwapeleka watanzania nchini Ufaransa kujiendeleza zaidi.Ni matarajio yetu Watanzania watachangamkia fursa hiyo ili kujifunza lugha hiyo," amesema.
Kwa upande wake Balozi wa Morocco hapa nchini ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Francphonie, Abdelilah Benrayane, amesema mahadhimisho hayo yataenda pamoja na matukio mbalimbali ikiwemo kuwainua wanawake katika maendeleo.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Tanzania ni wakati sahihi kwa watu wake kuanza kujifunza Kifaransa ambacho kinazungumzwa katika nchi nyingi Duniani na kwamba umoja wa nchi zinazozungumza lugha hiyo ulianza mwaka 1970.
Balozi wa Morocco nchini Tanzania ( wa tatu kulia) akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo anaendelea kuhamasisha Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa
Balozi wa Comoro nchini Tanzania Dk. Ahmamada El Badaoui Mohamed Fakih( wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kuzungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa nchi zinazoongea lugha Ufaransa
Balozi wa Belgium nchini Tanzania Peter Van Acker (wa pili kushoto) akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu nchi yao inavyohamasisha lugha ya Kifaransa ambayo ni moja ya lugha inayotumiwa na watu wengi
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier ( wa tatu kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaaam kuhusu maadhimisho ya miaka ya 50 ya Umoja wa Nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (Angro- phone). Wengine ni mabalozi wa nchi mbalimbali nchini ambao wanazungumza Kifaransa
Mabalozi wa nchi mbalimbali chini Tanzania ambao wako kwenye Umoja wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanyika kwa mkutano unaohusu maadhimisho ya miaka 50 ya umoja huo.
Baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania wakiwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...