Hali ya wasiwasi yatanda nchini Kenya baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kuthibitishwa kupitia Wizara ya afya.
Ijumaa, waziri wa Afya bwana Mutahi Kagwe alisema kwamba mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa na maambukizi hayo Alhamisi usiku.
Baada ya tangazo hilo, raia walionekana wakikimbilia kwenye maduka ya jumla kununua kemikali za kuua viini vya bakteria mikononi maarufu kwa kiingereza kama ''hand sanitisers'' pamoja na barakoa za kufunika uso.
Wateja walioanza kumiminika nyakati za mchana walikuwa na wakati mgumu kupata bidhaa hizo zilizokuwa adimu ghafla za kemikali za kunawa mikono zinazoua viini mara moja na barakoa.
Mteja mmoja aliyetembelea duka la jumla alihakiishiwa kwamba bidhaa hizo zitapatikana asubuhi ya leo kwa sababu zimeagiza kwa wingi lakini pia akaombwa kufika mapema kwasababu ni bidhaa zinazokimbiliwa na wengi.
Baadhi ya wateja walilazimika kununua bidhaa zingine mbadala za kuua viini mfano wa zile zinazotumika wakati wa kuosha nguo mara nyingi ikiwa ni zile za watoto wadogo, lakini wakati huu zikilengwa kumimininwa kwa kaisi kidogo katika maji ya kunawa mikono au kuosha sakafu.
Licha ya kwamba, maduka ya jumla na yale ya kuuza dawa yameahidi upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa kiwango kikubwa, baadhi ya wateja wanahofia kwamba huenda bei za bidhaa hizo ikapanda maradufu kwasababu ya uhitaji wake wakati huu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...