Benki ya Dunia imeanza ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ukarabati wa reli ya kati - TIRP kuanzia Dar es Salaam Kuelekea Isaka - Tabora, hivi karibuni, Machi 2020.

Benki hiyo ambayo ni wafadhili wa ukarabati wa mradi wa reli ya kati, hufanya ukaguzi mara kwa mara kwa lengo la kujua kiwango na ubora wa nyenzo zinazotumika ili kukamilisha ukarabati huo.

Mtaalamu wa maswala ya elimu ya mazingira kutoka Benki ya Dunia Bi. Elina Kashangaki amesema kuwa wanafarijika kuona kwamba kazi inakwenda vizuri ambapo ni asilimia takriban 76 za ukarabati tayari zimekisha fanyika na kubaki vipande vidogo vyakumalizia ili kufikia tamati ya ukarabati huo.

“Kiukweli tumetembea na tumejionea wenyewe jinsi ukarabati unavyoendelea na kipande kikubwa hata treni ikipita haiyumbi kama ilivyokuwa awali" alisema Bi. Elina Kashangaki .

Ziara hiyo ya ukaguzi ambayo imeanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na kuendelea mpaka Isaka - Tabora, ambapo wageni hao wakiambatana na wahandisi washauri kutoka kampuni ya DOWHA pamoja na baadhi ya wahandisi na wafanyakazi kutoka TRC watakagua  maeneo yote ya reli ya kati yaliyokamilika na ambayo ukarabati bado unaendelea.

Msaidizi wa afisa jamii wa mradi Bw. Askari Shengena amesema kuwa kufanya ziara hiyo ya ukaguzi kuna umuhimu sana kwa upande wa ujenzi wa reli pamoja na kuona changamoto zilipo baina ya watu na miundombinu ya reli ili kuweza kuhakikisha miundombinu ya reli inadumu kwa muda mrefu .

“Tunafanya kazi kubwa ya kuelimisha umma juu ya athari ya kufanya shughuli kandokando ya njia za reli  pamoja na kushauri nini kifanyike katika ukarabati wa ujenzi wa reli “ , alisema Bw. Shengena.

Moja ya vitu vinavyokaguliwa ni ukarabati wa madaraja , uwekaji wa mataruma mapya na kutoa ya zamani, ujenzi wa mitaro pamoja na uboreshwaji wa kiwango cha reli katika usafirishaji.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...