Na mwandishi wetu, Arusha
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoani humo kuendelea kutenga asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuwaepusha na ukatili wa kijinsia.
Ametoa agizo hilo jana tarehe 04/02/2020 wakati akizindua Msafara wa Kitaifa wa kijinsia wa kutokomeza ukatili katika eneo la Ngaramtoni Mkoani Arusha.
"Tumeona njia moja ya kumsaidia mwananchi ni pamoja na kutenga fedha za kuwasaidia kina mama, vijana na watu wenye ulemavu. Nizielekeze Halmashauri zetu kuendelea kutenga fedha hizo ziweze kuwafikia kwani ni mkakati wa nchi yetu katika kuwakomboa na ukatili" amesema Kwitega.
Ameongeza kuwa, Serikali na Wadau wana wajibu wa kushirikiana kutoa elimu ya mara kwa mara na kwa njia tofauti ili kufikisha ujumbe kwa jamii kuhakikisha kwa pamoja vitendo vya ukatili vinazuiliwa.
"Ni matumaini yangu kupitia msafara huu, kila mmoja aliyepo hapa atakuwa ni balozi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake" Amesema Kwitega.
Ametoa wito pia kwa Jeshi la Polisi Mkoani humo kuendelea kushirikiana na wadau wengine kupitia madawati ya kijinsia kuwabaini waathirika na kuwasaidia.
Ametoa rai pia wadau kuongeza vituo vya huduma ya pamoja ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Naye Afisa maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Hanifa Selengu amesema lengo la msafara huo ni kutoa elimu kwa wananchi kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia wa aina zote.
Akitoa elimu kwa wananchi kuhusu ukatili wa kijinsia Afisa Bw. Seto Ojwang amewaasa wananchi kukataa mila na desturi kandamizi kwa wanawake kwani zina madhara mengi ikiwemo kupunguza nguvu kazi ya kuchangia pato la familia na Taifa kiuchumi, kutojiamini na magonjwa yanayotokana na msongo wa mawazo.
Amewahimiza wanawake kutoa taarifa za ukatili kwenye madawati ya jinsia yaliyo kwenye vituo vya Polisi nchi nzima.
Mwanasheria kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Idda Mbogoro jamii nzima ina wajibu wa kulinda usalama wa watoto ili wasiathirike na ukatili wa kijinsia.
Wizara ya Afya, chini ya Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Wadau inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kupitia misafara ya Kitaifa ya Twende pamoja, kwenye baadhi ya Mikoa nchini ambapo msafara kuanzia Mikoa ya Arusha, Manyara, Mwanza na Simiyu umeanza jana tarehe 04/03/2020.
Msafara huo utahitimishwa Mkoani Simiyu ambapo kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yatafanyika tarehe 08/03/2020.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Hanifa Selengu akieleza lengo la msafara wa Kitaifa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wananchi waliojitokeza wakati Msafara huo ulipozinduliwa mapema jana kwenye eneo la Ngaramtoni Mkoani Arusha.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Idda Mbogoro akitoa mada kuhusu haki na wajibu wa mtoto wakati wa uzinduzi wa msafara wa kutokomeza ukatili wa Kijinsia Mkoani Arusha hapo jana eneo la Ngaramtoni.
Wanawake wakicheza kwa pamoja wimbo maalum wa Wanawake wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye eneo la Ngaramtoni Mkoani Arusha hapo jana.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega akizungumza na wananchi wa Ngaramtoni Arusha wakati akizindua Msafara wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili unaoanzia Mkoani Arusha na kupita katika Mikoa ya Manyara, Mwanza na Simiyu.
Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Seto Ojwang akitoa elimu kuhusu Ukatili wa kijinsia kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha hapo jana wakati Msafara wa kutokomeza ukatili ukiwa Mkoani hapo eneo la Ngaramtoni.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili, wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali katika eneo la Ngaramtoni hapo jana

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...