Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania
PLC Wakishiriki zoezi la kupanda miti katika Hospitali ya Muhimbili
eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea katika
hospitali hiyo kwa ajili ya kuwapa pole wagonjwa ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Meneja chapa na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania PLC, Grace Kijo akipanda mti katika eneo la Hospitali
ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, wakati walipotembelea wagonjwa
katika Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake
Duniani 2020.
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kushoto) pamoja na muuguzi
wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, Christina Mwandaliwa
wakishirikiana kupanda mti wakati wafanyakazi wa Vodacom
walipotembelea katika Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
siku ya Wanawake Duniani 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Muhimbili eneo la Mloganzila jijini
Dar es Salaam, Redemptha Matindi (kushoto) akimshuhudia Meneja Ruzuku na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akipanda mti
wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea katika Hospitali hiyo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Muhimbili eneo la Mloganzila jijini
Dar es Salaam, Redemptha Matindi (kulia) akiongea na waandishi wa
habari wakati wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, walipotembelea
katika wodi za wagonjwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya
Wanawake Duniani 2020 (wapili kulia) ni Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald.Pia wafanyakazi hao
walipanda miti katika eneo la Hospitali .
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam,
Redemptha Matindi (katikati) akiteta jambo na Meneja Ruzuku na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, wakati
wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika Hospitali
hiyo na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake
Duniani 2020.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania
PLC, wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea Wagonjwa na
kupanda miti katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam,
Redemptha Matindi (katikati) akimshuhudia Meneja Ruzuku na Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimjulia hali mmoja wa
akina mama aliyelazwa katika Hospitali hiyo wakati wafanyakazi wa
kampuni ya Vodacom walipotembelea wagonjwa na kupanda miti ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2020.
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimjulia hali mmoja wa
akina mama aliyalazwa katika Hospitali Mloganzila jijini Dar es
Salaam,wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa na
kupanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...