Kesi ya jinai inayomkabili mfanyabiashara ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT-CCM Wilaya ya Kinondoni, Frolence Masunga (45) mkazi wa Kimara Suka jijini Dar es Salaam imeahirishwa tena.
Kesi hiyo imetajwa kwa mara ya pili mnamo Machi 9,2020 ambapo ilishatajwa kwa mara ya kwanza Januari 22,2020 katika mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu mfawidhi Martha Mpanze.
Masunga anashtakiwa kwa Kosa la kuchukua fedha za Abdallah Majura Bulembo, kwa njia ya udanganyifu, ambapo imeelezwa kuwa mnamo Disemba,2019 katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam Masunga alipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Shilingi millioni 100 kutoka kwa Bulembo kwa lengo la kumuuzia nyumba iliyopo Kinyerezi ndani ya manispaa ya ilala, ambapo baadae hakuweza kukabidhi nyaraka za nyumba hiyo kwa Bulembo hivyo nyumba hiyo kuendelea kubaki mikononi mwake.
Kesi hiyo imeahirishwa ambapo imetajwa kusikilizwa tena machi 25/2020 mahakamani hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...