Mkufunzi wa chuo cha Teknolojia stahiki ya nguvu kazi ATTI mbeya Richard Kansimba akiwafundisha kwa vitendo wanawake waliokuwa kwenye mafunzo ya ujenzi na ukarabati wa barabara yaliyofanyika mkoani Morogoro namna ya kufanya vipimo vya barabara na kuweka usawa ili kuepukana na matuta yasiyo yalazima barabarani.
Washiriki wa mafunzo ya ujenzi na ukarabati wa barabara wakijifunza namna ya kutumia kipimo cha mkanda (Tap Measure) kupima usawa wa barabara wakiwa katika eneo la chuo cha ujenzi mkoani Morogoro.
Wanawake wakishiriki mafunzo ya ujenzi na ukarabati wa barabara mkoani Morogoro wakijifunza kwa vitendo mafunzo waliopewa ya ujenzi wa barabara kwa kufuata vipimo, (pichani wanasawazisha udongo ili kupata usawa wa barabara).
Mkufunzi wa chuo cha Teknolojia stahiki ya nguvu kazi ATTI mbeya Richard Kansimba akielezea namna ambavyo barabara inatakiwa kuchongwa mara baada ya kupima bila kuathiri kamba zilizonyoshwa kwenye vipimo hivyo.
Wanawake walioshiriki mafunzo ya teknolojia stahiki ya kutumia nguvu kazi yaliyofanyika mkoani Morogoro wakiwa wamesimamisha vibao kuangalia usawa wa barabara ambayo inatakiwa kuchongwa mara baada ya vipimo .
Wanawake baada ya kufanya vipimo vya ujenzi na ukarabati wa barabara na kujilizisha na vipimo hivyo wakiwa wameenza kuchonga barabara hiyo ambayo walikuwa wakipima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...