Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (waliokaa Katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi
wa Dini na Serikali pamoja na Watumishi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF).
Meneja wa NHIF, Dkt. Janet Pinda
akitoa elimu juu ya huduma ya vifurushi vya Bima ya Afya mbele ya Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo pamoja na Wakurugenzi wa
halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Viongozi wa Dini.
Meneja wa NHIF, Dkt. Janet Pinda.
…………………………………………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Mkoa huo kutafakari
namna ya kujali na kuwekeza katika afya kwa kutahadharisha kuwa kufanya
hivyo ni jambo lisiloepukika ili kuweza kutimiza malengo ya kuimarisha
afya zao na hatimae kujizatiti katika kuujenga uchumi wa mkoa kuanzia
katika ngazi ya familia na hivyo kuwataka kujiunga na huduma za bima ya
afya zinazotolewa na serikali nchini.
Amesema
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikifanya maboresho mbalimbali
katika huduma za Afya ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na Afya
njema ambapo kwa kupitia Wizara ya Afya iliweza kuboresha Mfuko wa
Huduma ya Afya ya Jamii (CHF) kutoka kutibiwa mahala ulipokatia kadi
hadi kupata huduma kupitia kituo chochote cha kutolea huduma za afya
nchini.
Aidha, ameongeza
kuwa kutokana na takwimu za mkoa wa Rukwa kuwa chini katika kujiunga na
mifuko hiyo amewataka, Wakurugenzi wa halmashauri, Wakuu wa Wilaya,
atumishi wa vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kuwaomba Viongozi
wa Dini kuhamasisha wananchi wengi zaidi kujiunga na huduma mpya ya
vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kupata huduma
bora na ya wakati.
“Katika kipindi
cha nusu mwaka wa 2019/2020 Mkoa wa Rukwa ulilenga kusajili wanachama
1,287 wa NHIF wasio Watumishi wa Serikali, lakini Wanachama
waliosajiliwa ni 437 ambao ni sawa na asilimia 34 ya lengo. Kwa upande
wa huduma ya vifurushi vya NHIF tangu mpango huu uzinduliwe Wanachama 15
tu wameandikishwa kati ya Wanachama 523 waliolengwa kuandikishwa sawa
na asilimia 2.8 (2.8%),” Alisema.
Halikadhalika,
Amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanawasilisha michango
ya watumishi wao wanaolipwa mishahara kwa mapato ya ndani pamoja na
waheshimiwa madiwani ili kuepuka kuzorotesha juhudi kubwa zinazofanywa
na serikali juu ya kuboresha huduma za afya kwa watumishi na viongozi
wake na kuonya kuwa kutofanya hivyo kutasababisha huduma zao kusitishwa
hali itakayopelekea fedheha kwa watumishi na waheshimiwa madiwani.
Mh. Wangabo
ameyasema hayo katika ufunguzi wa kuitambulisha rasmi huduma ya
vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya katika semina
iliyowajumuisha Wakurugenzi wa halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa
Dini pamoja na wataalamu wa sekta ya Afya ngazi ya mkoa
Wakati akitoa
maelezo juu ya huduma hiyo ya vifurushi Meneja wa NHIF Mkoa wa Rukwa
Dkt. Janeth Pinda amesema kuwa tangu kuzinduliwa kwa huduma hiyo
wamekuwa wakitoa elimu kuanzia ngazi ya mtaa, vijiji na kata na hatiame
kufanya semina na viongozi wa juu katika ngazi ya mkoa ambao wana
ushawishi mkubwa kwa wananchi ndani ya mkoa na kwa kufanya hivyo
kutawawezesha kufikia malengo ya serikali katika kutoa huduma bora kwa
wananchi na hivyo kuomba ushirikiano kutoka kwa viongozi hao.
“Kuanzishwa hasa
kwa hivi vifurushi vipya ilikuwa ni kuongeza wigo wa wananchi katika
mfumo wa bima ya afya, kwasababu kama inavyofahamika kwa hapo awali
ilikuwa kwa wananchi ama wafanyakazi ambao wako katika sekta rasmi,
lakini wale ambao hawakuwa katika sekta rasmi haikuwa rahisi kuwafikia
ili waweze kupata huduma za bima ya afya,” Alisema.
Hata hivyo
alisema kuwa nia ya mfuko huo ni kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na
elimu ya afya ili aweze kuona umuhimu wa kuwekeza katika afya na
kueleza kuwa mfuko huo mfuko huo kwasasa unatoa huduma kwa wananchi wote
kwa kuangalia kipato cha muhusika huku wakiwa na kauli yao kuwa
“Tumekufikia, Jipimie”.
Ili kuongeza wigo
wa wananchi katika mfumo wa bima ya afya, NHIF imeanzisha vifurushi
vipya vya bima ya afya vyenye majina ya Najali Afya, Wekeza Afya, na
Timiza Afya ambapo kwa kufanya hivyo mwananchi miongoni mwa huduma
nyingine nyingi mwananchi anaweza kupata aina 27 za huduma za upasuaji
mdogo na aina 14 za huduma za upasuaji mkubwa katika kifurushi cha
Najali Afya ambacho ndio kifurushi cha chini kwa bei ya Shilingi 192,000
kwa mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...