Kikao cha kujadili tishio la
ugonjwa wa corona baina ya Serikali na shirika la afya duniani, Mabalozi
na wakuu wa taasisi za kimataifa na wadau wa sekta ya afya
kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya afya jijini Dar
es salaam
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa (UN) Zlatan Milisic akichangia kwenye mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kutoka mashirika na taasisi wakifuatilia mkutano huo
Waziri Ummy Mwalimu akiongea kwenye kikao kilichojadili kwa pamoja tishio la mlipuko wa ugonjwa wa corona
Mkurugenzi wa idara ya dharura na
maafa kutoka wizara ya afya Dkt. Elias Kwesi akiwasilisha mada kwenye
kikao cha kujadili kukabiliana na Corona
Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula akiongea kwenye kikao hicho
Mratibu wa dharura na maafa kutoka WHO akiwasilisha mada
………………………………………………..
Na. Catherine Sungura-Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya na
wadau wa sekta ya afya ikiwa na lengo la kujadili kwa pamoja tishio la
mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Waziri Ummy amesema kikao hicho
waliwaeleza wadau kama taarifa ya shirika la afya duniani(WHO)
ilivyotangaza hali ya maambukizi ya ugonjwa huo duniani hivyo kama
serikali ni vyema kuwapatia taarifa wadau hao
“Tumewapa taarifa wadau wetu na
kuwahakikishia kwamba tanzania hakuna mtu mwenye maambukizi mwenye
maambukizi ya virusi wa corona na tumewaeleza hatua gani kama serikali
tumezichukua katika kujiandaa kukabiliana na tishio hili”.
Katika kikao hicho waziri
ameeleza kwamba wizara yake imeweza kuchukua hatua ya kukabiliana na
tishio hilo kwa kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo mbali mbali ikiwemo
kwenye viwanda vya ndege na viingilio vingine ikiwemo bandarini.
Hata hivyo Waziri Ummy amesema
kwamba wameweza kutoa mafunzo kwa baadhi ya wataalamu wa afya waliopo
mikoani pamoja na kuandaa dawa, vifaa na vifaa tiba endapo nchi itapata
mshukiwa wa virusi vya corana.
“Tumewaomba washirikiane nasi
katika kuhakikisha kwamba sasa tunakua tayari kukabiliana na tishio hilo
hata kama hatuna mgonjwa hii tulikuabaliana kwenye mkutano wa nchi
wanachama wa SADC kwamba nchi zote tunaingia kwenye hatua ya
kukabiliana”.Alieleza Waziri Ummy.
Katika kikao hicho amesema kuwa
wamewaomba wadau waunge mkono katika kutoa mafunzo zaidi hususan kwa
wataamu wote wa afya ili kuwakinga na maambukizi pamoja na kutoa elimu
na taarifa sahihi kwa wananchi nchini.
Wadau hao wameishukuru serikali
kupitia wizara ya afya kwa kuwashirikisha na wameridhika kwa hatua
zilizochukuliwa katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huo.Kikao hicho
kiliwashirikisha shirika la afya duniani(WHO),Mabalozi na Wakuu wa
taasisi za kimataifa hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...