-Wafanyakazi bora kitengo cha mauzo nao wapatiwa tuzo
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya Kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, imekutana jijini Dar es Salaam na wasambazaji wa bidhaa zake kutoka nchini pote kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuboresha zaidi usambazaji sambamba na kuwashukuru ambapo wasambazaji bora 2 wamejipatia zawadi ya magari ya kubeba mizigo kwa ajili ya kurahisisha usambazaji wa bidhaa kwa wateja na wasambazaji wengi wamejipatia vyeti na vikombe vya kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.

Mbali na wasambazaji wafanyakazi wa kitengo cha mauzo wa TBL, nao wamezawadiwa tuzo kutokana na kazi nzuri wanayoendelea kufanya katika kufanikisha malengo ya kampuni ya kuendelea kuwa kampuni bora ya bia inayoongoza nchini.
 Wasambazaji katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TBL,Philip Redman (katikati) baada ya kukabidhiwa zawadi na tuzo
  Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kulia) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari Happyness Joseph (Katikati) kutoka Fresa Investment baada ya kuibuka msambazaji bora mwaka 2019 na kujishindia lori la usambazaji.
 Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kushoto) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari Richard Justine kutoka Mbeya baada ya kuibuka

 Baadhi ya wafanyakazi wa matzo wakifurahi na Mkurugenzi Mkuu baada ya kushinda tuzu

Wafanyakazi wa kitengo cha mauzo wakionyesha tuzo zao katika hafla hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...