BENKI ya TPB imesaidia umaliziaji wa ujenzi wa kituo cha afya Mtii, kilichopo Kata ya Mtii, Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro. Kituo hicho cha afya kinajengwa na jamii ya wanakijiji wa Mtii chenye vijiji vitatu na vitongoji kumi.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyamule, ameipongeza benki ya TPB kwa msaada mkubwa ilioutoa kwa ajili ya kumalizia eneo la OPD la kituo hicho ili kianze kutoa huduma kwa jamii. “Natoa shukrani zangu zadhati kwa benki ya TPB kwa msaada wenu wa kuwezesha kukamilisha eneo hili la OPD. Naamini sasa wananchi wataanza kupata huduma za OPD hapa badala ya kutembea kilomita 10 kwenda kwenye hospitali ya KKKT Gonja kama walivyokuwa wakifanya hapo awali”, amesema Senyamule.
Kwa upande wake Meneja wa benki tawi la Arusha Ayubu Mkwawa amesema benki ya TPB inatambua umuhimu wa Watanzania wote kupata huduma bora za afya na hivyo haikusita kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho cha Mtii kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 25 kwa ajili ya kusaidia ujenzi huo, hasa baada ya kuona umuhimu mkubwa wa kuwa na kituo cha afya katika kijiji hicho baada ya wakazi wa kijiji hicho kutembea umbali mrefu ili kupata huduma za afya. Pia aliwapongeza wakazi wa Mtii kwa juhudi zao za kuchangia ujenzi huo kwa asilimia 95 na pia kwa usimamizi mzuri wa ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyama aliambatana na viongozi mbalimbali wa Wilaya hiyo pamoja na viongozi wa benki ya TPB ili kuona maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho ambacho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi hivi karibuni.

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule akitoa pongezi kwa benki hiyo kutokana na uamuzi wake wa kusaidia ujenzi huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...