Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani akikagua miundombinu ya Dalaja la mto Kilombero kabla ya kufika katika kituo cha kuzalisha umeme cha kidatu Mkoani Morogoro.
Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alipofanya ziara katika bwawa la Mtera.
Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani akikagua mitambo katika kituo cha kuzalishia umeme cha kidatu Mkoani Morogoro,akiwa katika ziara yake ya kukagua vituo vya kuzarisha umeme hapa nchini.
Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Morogoro na Iringa katika vituo vya kuzalishia umeme vya Kidatu na Mtera akitoa katazo la kuwepo kwa
mgao wa umeme hapa nchini.
Na Farida Saidy Morogoro.
Kufuatia Baadhi ya Mikoa hapa nchini kukosa umeme wa uhakika Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amefanya ziara ya kukagua vituo vya kuzalishia umeme Kidatu Mkoani Mororgoro ikiwa na kituo cha Mtera Mkoani Iringa kwa lengo la kubaini chanzo cha kukosekana na kwa umeme katika mikoa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Waziri Kalemani Mara baada ya kutembelea vituo hivyo amewata viongozi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO kuacha tabia ya kutoa mgao wa umeme kwa wananchi, na kusema kuwa Tanzania inaumeme wakutosha hivyo hatarajii kuona kuna mkoa hauna umeme kwa kigezo cha upungufu wa umeme.
Hata hivyo Waziri Kalemani ikiwa katika kituo cha uzalishaji wa umeme Mtera mkoani iringa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba Kuhakikisha anamchukulia hatua mfanyakazi Abubakari kwa kosa la kuagiza mkoa wa Mwanza uwe na mgao wa umeme bila sababu za msingi.
“Usipomchukulia hatua huyu mfanyakazi anaeitwa Abubakari basi Mimi nitajua nani wa kumchukulia hatua kwa kuwa tatizo hilo kwa Abubakari limekuwa likijirudia mara kwa mara” alisema Waziri Kalemani “haiwezekani mtu mmoja anaamua kutoa maagizo ya kuwepo mgao
wakati hakuna tatizo lolote lile”alisema Waziri Kalemani .
Alisema serikali imejenga nyumba za wafanyazi pale ubongo kwa ajili ya uangaliangalizi wa mwenendo wa umeme nchi nzima lakini bado wafanyakazi wanakaidi kukaa hapo jambo linalopelekea ufanisi wa kazi kuwa hafifu.
katika hatua nyingine Dkt. Kalemani alitoa tahadhari kwa wananchi waliokaribu na mto ya Ruaha mkuu pamoja na kilombero kuchukua tahadhari ya kundoka katika maeneo hayo hususani katika kipindi hiki ambacho maji yanafunguliwa katika mabwawa ya kuzalishia umeme.
“tumeona ni muhimu kutoa tahadhari kwa Wananchi kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha, kwa kawaida Bwawa la Mtera kulijaza
huchukua miezi 3 hadi 4 kwa mvua za masika, lakini kwa kipindi hiki
mvua za vuli zimekuwa nyingi ndani ya mwezi mmoja hivyo kina
kimeongezeka”, alisema Dkt. Kalemani.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema
kuwa wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara kwa wananchi kwa
lengo la kuwaokoa na madhara ambayo wanaweza kuyapata kipindiki
cha mafuriko hasa wale wanaofanya shughuli katika bwawa la Mtera na
kandokando ya mto Ruaha.
katika hatua nyingine Kasesela alimuomba waziri kusaidia kuharakisha
ujenzi wa daraja jipya ambalo michoro yote imekamilika ila fedha bado
hazijapatika kwa lengo la kuliokoa daraja lililopo kutokana na magari
yanayopita hapo yanauzito mkubwa sana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...