Katika kuhitimisha  mwezi wa siku ya wanawake duniani Jeshi la Magereza Tanzania limewashukuru wanawake wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa moyo wa upendo walioonyesha kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali  kwajili ya wafungwa wanawake katika gereza la Segerea.

Shukrani hizo zimetolewa wakati wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali ambavyo ni simenti mifuko 20, sabuni ya unga mifuko mikubwa miwili, ndoo za maji ya kunywa 10, sabuni za miche katoni 2, Dawa za meno mabox 2, miswaki mabox 2, taulo za kina mama za kujihifadhi katoni 4 na sabuni za kunawa mikoni katoni 1  ili kuwawezesha wafungwa wanawake wa Gereza la Segerea kutatua shida mbalimbali zinazowakabili  katika gereza hilo  jijini Dare s salaam hapo jana.

Akitoa salam za awali  Afisa asilimali watu Bi, Asia Shio kwa niaba ya Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege  Tanzania amelishukuru Jeshi la Magereza kwa kuweza kutoa nafasi ya kukabidhi vifaa hivyo huku akieleza kuwa wakati ujao vitapelekwa  vifaa vyote muhimu vinavyoitajika mpaka kwa watoto wachanga waliopo katika gereza hilo kwani mara baada ya kufika katika gereza hilo wamegundua kuna uhitaji mkubwa zaidi.

Awali akitoa maelezo ya kutoa msaada huo kwa wafungwa wanawake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Tughe Makao Makuu Bi,  Pendo Mwakilasa alisema  kwa niaba ya  wanawake wa Makao Makuu ya TAA  na Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nerere (JNIA) imekuwa faraja kuweza kupeleka msaada huo.

“ Tumemeguswa na maisha ya wafungwa hawa  wanawake haswa wanaoishi na watoto wachanga   na  tumeleta  vifaa hivi ili  viweze kuwasaidia huku tukiendelea kujichanga kuweza  kuleta vifaa vingine kwani tunaamini hii itakuwa ni sehemu tu ya kupunguza shida ndogondogo”, alisema.

Kwaniaba ya wafungwa hao Wanawake Mkuu wa gereza  hilo  Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP George Wambura aliwashukuru sana Wafanyakazi Wanawake wa TAA kwa kugushwa kwa namna moja au nyingine kwa kukumbuka kupeleka  mahitaji hayo muhimu kwaajili ya wafungwa hao na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo huo wa upendo na utoaji.

Naye Kiongozi wa Gereza la Wanawake SSP Theopista Gauza anaejulikana kama Bibi jela alisema hana  namna ya kuwashukuru kwa vifaa hivyo kwaajili ya wafungwa wanawake anajua TAA  wameguswa  mpaka kuweza kutoa sehemu hiyo ya msaada japo havitatosheleza  lakini vitawasaidia kwa wakati huu. 

“ Si  wafungwa wote waliomo humu ni watu wabaya ila wapo kulingana na utaratibu wa kisheria na gereza hili linawafungwa zaidi ya elfu 3000 wakiwemo watoto wachanga walio chini ya miaka 3 hivyo mtaona ni jinsi gani uhitaji wa vitu mbalimbali mpaka kwa hawa watoto wadogo unahitajika”, alisema.

Halikadhalika  alisema watoto waliopo  magerezani wana mahitaji ya msingi sana kama maziwa, nepi za kutupa (pampers), nguo na vinginevyo  ili kuweza kuwastiri  kwani si wafungwa wote wenye ndugu katika Jiji hili hivyo wanamahitaji wanayo yakosa kwa kiasi kikubwa,

“Ila nasikitika kwa leo hamtaweza kuwaona kwani kutokana na ugonjwa wa covid _19 unaotokana na kirusi cha Corona imezuiliwa kuingia ndani ya gereza na kusalimiana nao ila vifaa vyao tutavifikisha kwa niaba,”. Alisema

Katika hatua nyingine Staff Sajenti (SSGT) Hamis Twalib  alisema   Jeshi hilo  linashukuru kwa vifaa hivyo kwaajili ya wafungwa wanawake lakini pia msaada huo utasaidia Jeshi kuweza kuangalia mahitaji mengine kwani mahitaji mengine ya msingi kwasasa yatakuwa yameshapatikana.

Msaada huo uliopelekwa kwa wafungwa wanawake ni sehemu ya kuendelea  kuadhimisha kilele cha siku ya Wanawake Duniani  ambayo ilikuwa tarehe 8 mwezi huu wa machi ukiwa umetokana na mchango  kutoka kwa baadhi ya Wanawake wa TAA Makao Makuu na Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mahusiano Bi Pamela Mugarula akikabidhi moja ya kifaa cha msaada kwa  Mkuu wa Gereza la Segerea ACP George Wambura kwaajili ya wafungwa Wanawake katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  Wafanyakazi  Wanawake wa TAA Makao Makuu na JNIA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa gereza wa wanawake SSP Theopista Gauza ( Bibi jela) wakati wa utoaji wa msada kwa wafungwa wanawake katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa TAA na Viongozi wa Gereza la Segerea  wakiwa pamoja na  vifaa vya msaada vilivyowasilishwa kwaajili ya Wanawake wa gereza hilo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...