Na Yassir Simba,  Michuzi Tv

Mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga uliopigwa leo katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam  umemalizika kwa Yanga timu ya wananchi kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0

Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 11:00 jioni uliamuliwa kwa adhabu ndogo yaani free nje kidogo la lango la Simba mara baada ya kiungo wa Simba Jonas Gerald Mkude kumfanyia madhambi Benard Morrison katika dakika ya 43 ya mchezo ndipo muamuzi wa mchezo huo kutoka Morogoro Martin Sanya kuamuru mpira wa adhabu upigwe kuelekea lango la Simba na winga machachari wa Yanga Benard Morrison kuukwamisha mpira huo kimiani baada ya golikipa wa Simba Aishi Manula kushindwa kuucheza mpira huo na kupelekea Yanga kupata bao la kuongoza hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba wakitafuta bao la kusawazisha na Yanga wakijilinda ambapo dakika ya 65 Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa mfungaji wa bao Benard Morrison na kuingia Patrick Sibomana huku Simba ikifanya mabadiliko ambapo dakika 75 Simba   ya kumtoa Meddie Kagere na kuingia Hassan Dilunga

Licha ya mabadiliko yalifonywa na timu zote mbili firimbi ya mwisho ya muamuzi kutoka mkoani Morogoro Martin Sanya katika dakika ya 95 iliwafanya Yanga kumaliza ukame wa kutoka kushinda kwa miaka minne katika mechi za 'Derby'.

Rasmi Simba anasalia nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na alama 68 baada ya kucheza michezo 27 huku Yanga wamepanda kutoka nafasi ya nne kwenda ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa na Alama 50 mara baada ya kucheza michezo 25.






















 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...