Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kujitahidi kuendesha kwa spidi ujenzi wa Hospitali mbili za Uhuru na Mlolo.

Jafo amesema kukamilika kwa haraka kwa ujenzi wa Hospitali hizo kutatoa fursa nzuri kwa wananchi wa Chamwino kupata huduma bora za kiafya.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua hospitali hizo, Jafo amesema ujenzi wa hospitali hizo umeenda kwa spidi inayotakiwa hivyo kuwa na imani zitaanza kufanya kazi ndani ya muda mfupi.

Amesema kukamilika pia kwa hospitali hizo kutasaidia pia kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona ambao umekua hatari nchini na duniani kwa ujumla.

" Niwapongeze sana kwa namna ambavyo mmekwenda na spidi inayotakiwa na Serikali yetu, Mhe DC nikupongeze sana wewe na timu yako. Hii inaonesha maagizo yangu niliyoyatoa mara ya mwisho yametekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Ndugu zangu hospitali hizi licha ya kwamba zitahudumia wananchi wa Chamwino na maeneo jirani lakini hata kwa kipindi hiki cha Corona bado zitaweza kutumika kusaidia wananchi ambao watapata maambukizi ya ugonjwa huo.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwataka viongozi hao kujilinda na ugonjwa wa corona pamoja na kutoa elimu kwa wananchi namna gani ambavyo wataweza kujikinga na maambukizi yake ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na kuvaa barakoa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga wakati alipofanya ziara wilayani hapo kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Hospitali mbilizi za Uhuru na Mlolo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo (kulia) akikagua ujenzi wa hospitali ya Mlolo wilayani Chamwino, Dodoma leo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Mlolo na Uhuru leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...