Baadhi ya waumini wakiwa katika Ibada ya pasaka katika kanisa Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Mlandizi Dayosisi ya Magharibi na Pwani Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya waumini wakiwa katika Ibada ya pasaka katika kanisa Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Mlandizi Dayosisi ya Magharibi na Pwani wakiwa wamekaa bila kusongamana.Picha na Vero Ignatus.
Na.Vero Ignatus ,Mlandizi Pwani
Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka inayoonyesha upekee wa Imani ya Kikristo duniani Jamii imetakiwa kujikita katika kijiandaa na kujiwekeza katika uchumi ili kuleta mabadiliko katika Maisha yao na kuwaandaa wanapofika katika Maisha ya uzeeni wasije kutaabika bila kuwa na msaada.
Hayo yamesemwa na mchungaji Ombeni Mlimi alipokuwa akihubiri katika ibada ya pasaka katika Usharika wa Mlandizi Dayosisi ya Magharibi na Pwani na kusema kuwa watu wengi wapo katika hali walizonazo sasa kwasababu ya Maisha waliyoyachagua kuishi.
Akizungumza katika kumbukumbu ya kufufuka kwa Yesu amesema kwamba ni ishara ya ushindi , nguvu hiyo ya ufufuo huo unaondoa hofu na changamoto ambazo zinazoweza kumzuia mwanadamu asiwe na mawasiliano mazuri na muumba wake
Aidha alisema kuwa Kristo mfufuka analifundisha Kanisa ujasiri na unyenyekevu wa hali ya juu kwani alijua mazingira na mipango ya kumuua na vikao mbalimbali ,ila ulipofika utimilifu wa wakati alifufuka kama alivyosema
Sambamba na hayo amewataka waumini hao kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) kama ilivyoagizwa na Wizara ya Afya ,pia
waepuke taarifa za mitaani kwani zinapotosha na siyo sahihi mara nyingi zinazidisha hofu kwa jamii badala ya kufuata maelekezo
Akinukuu maandiko matakatifu katika Biblia kitabu cha 1nyakati 12:32 aliwataka washarika hao kuwa na akili na kutambua nyakati hivyo amewataka wasiwe na wasiwasi kupindukia badala yake wafuate taratibu na maelekezo ya kitabibu Mungu atawaepusha na changamoto hiyo
Aidha katika ibada iliyofanyika siku Jumapili kwaajili ya sikukuu ya Pasaka usharikani hapo uongozi wa kanisa hilo uliweka utaratibu kwa kila mshirika kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kabla na baada ya kuingia Ibadani
Pia amewataka wazazi kuwa makini katika kipindi hiki cha likizo na kuhakikisha watoto wao wanaendelea kusoma wawapo majumbani,kwani pamoja na changamoto zote zilizopo bado watahitajika kurudi shuleni na mitihani itaendelea
‘’Najua baadhi yenu kukaa nyumbani ni mtihani lakini hakuna namna itabidi tu iwe hivyo kwaajili ya usalama wa afya zetu,kaeni na watoto wenu mzifahamu pia tabia zao,badhi yenu mlizoea kuamka asubuhi na kurudi jioni na wengine hata mabadiliko ya Watoto wenu hamyafahamu maana wengine wapo shule za bweni ’’
Amewasihi wazazi kuwasimamia watoto wao vyema na kuepuka kuwaacha huru na kuanza kuzuruka hovyo mitaani amesema kuwa serikali ilifunga shule ili wakae nyumbani na siyo mitaani kama inavyooneka sasa
‘’Wasimamieni Watoto wenu msiwaache huru wakaanza kuzurura hovyo mitaani,wasisitizeni kuhusu masomo, isijeikawa kuwa badala ya kusoma wanafunzi nmajikuta wazazi ndiyo mnasoma nyie kwa kutokuwatilia mkazo Watoto wenu’’
Wakati huo huo Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa leo Jumanne April 14,2020 katika kikao cha kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaotokana na maambukizi ya virusi vya corona( Covid -19) amesema hadi leo nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya Corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 4 ambao wote wapo jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...