Poleni na majukumu ya kazi huku tukiendelea kujikinga na janga hili la ugonjwa wa  COVID-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona

Nimeona ni vizuri  kuandika ujumbe huu mfupi kutokana na sintofahamu ya watu wengi  katika jamii yetu kuhusiana na baadhi ya vyakula kutibu ugonjwa wa COVID-19 .

Kutokana na janga hili watu wengi wamejikuta wakila kundi moja la vyakula kwa madai  ya kuuwa virusi vya  Corona. Kuna baadhi ambao wanaamini wakitumia juice za limao na tangawizi zitawasaidia kupona ugonjwa wa COVID-19.

Ukweli ni kuwa  matunda kama limao na mengine yote yenye uchachu ambayo ni jamii ya machungwa (citrus fruits), mapera, maembe, mananasi, ukwaju, ubuyu na grapes yana kiasi kikubwa cha vitamin C ambayo inasaidia  kuimarisha kinga ya mwili.

Utumiaji wa vyakula hivi utakusaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa yote sio COVID -19 pekee. Hivyo basi  utumiaji wa vinywaji hivi pekee hautakusaidia kukuponya na ugonjwa huu maana virusi hivi bado havina dawa isipokuwa ni kinga yako ya mwili pekee ndiyo inaweza kukufanya upate nafuu ya haraka endapo utapata maambukizi ya COVID -19.

Jambo la msingi  ni kuzingatia kanuni bora za lishe ikiwa ni pamoja na kufanya yafuatayo:

📌Pata mlo kamili wenye mchanganyiko wa  makundi muhimu yote ya chakula kama vile wanga kiasi, vyakula vyenye asili ya wanyama na mikunde, mafuta ya mimea,  mboga  za majani na matunda ya aina mbalimbali kama utaweza kupata bila kusahau maji ya kunywa safi na salama.

📌Fanya mazoezi kuimarisha zaidi afya yako sasa kama utatumia tu hizo chai na juice  ukalala siku nzima hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa hewa ni kubwa na kuwa rahisi kushambuliwa na virusi hawa. Jitahidi kufanya mazoezi hata dakika 30 tu kwa siku itakusaidia pia kuimarisha mfumo wako wa hewa na upumuaji.

📌Zuia msongo wa Mawazo. Kwa sasa hofu ni kubwa kulingana na historia ya ugonjwa wenyewe kama ilivyotokea katika mataifa yaliyotangulia kupata janga hili. Kweli hofu ni kubwa lakini ukikaa na kujipa mawazo zaidi unaharibu pia kinga ya mwili wako na kufanya rahisi kwako kushambuliwa na na virusi hawa.

📌Punguza matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara kwa sasa ili kuweza kulinda afya ya moyo wako na mapafu.

📌Kujifukiza na maji ya moto yenye mchanganyiko wa vitu vyenye harufu kama tangawizi, miarobaini, mkaratusi, mchaichai  nk itakusaidia kuzuia congestion kwenye airways ( inasafisha mfumo wa hewa) na  hata mafua ya kawaida njia hii inasaidia kurahisisha upumuaji. Virusi wanakawaida ya kupotea wenyewe kulingana na nguvu ya kinga yako ya mwili....

📌Jambo la mwisho na la muhimu  ni kuchukuwa tahadhari zote tunazoambiwa na wataalamu wa afya.

Maria Samlongo
Afisa Lishe
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)


Eat healthy stay safe.💞

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...