Toka kuingia kwa virusi vya coronavirus nchini njia mbalimbali zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa kuzuia kasi ya maambukizi.Taasisi za elimu zimefungwa, hoteli mbalimbali, mikusanyiko imezuiwa na kupungua kwa mfano Mapinduzi Day, na njia nyingi za kuelimisha umma zinafanyika kuhakikisha tunabaki salama.
Juhudi pia zinafanyika kuhamasisha kuhusu matumizi ya fedha kijitali (kulipa, kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu). Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), njia hii ya kutuma, kulipa na kupokea fedha inapunguza kukutana ana na kwa ana na pia kupeana fedha mikononi hivyo kwa namna moja au nyingine kusaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya corona.
Hata kabla ya janga la corona, fedha kwa njia ya simu tayari ilikuwa namna muhimu ya maisha yetu. Imekuwa njia ya uhakika kutuma, kupokea, kufanya malipo. Mwaka 2019 watumiaji wapya milioni 2 wa njia hii ya kifedha waliongezeka na sasa jumla ya watumiaji wanaelekea milioni 23.
Licha ya hili la kupambana kuzuia kuenea kwa maambukizi bado zipo faida nyingi za njia hii: mfano haikuhitaji kwenda benki kutoa na kuweka fedha. Mbali na hiyo pia ni njia salama ya kutuma na kupokea pesa ndani na nje ya Tanzania. Katika kupanua zaidi wigo huo na kufanya maisha yawe bora zaidi, wiki hii Tigo Tanzania imetangaza huduma mpya ambayo itakayowezesha watumiaji wake kutuma na kupokea fedha katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda na Rwanda.
Katika nyakati hizi za janga hili, inatia moyo kuona sekta ya mawasiliano ya simu ikiendelea kuwa bunifu na kutupa huduma kusaidia watu kuendelea kutuma na kupokea fedha kuendesha biashara na familia zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...