Mkurugenzi
 Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kulia) akipunga  mkono kwa 
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi 
Seif Ali Iddi (haonekani pichani) wakati akikabidhi kiasi cha shilingi 
milioni 300 kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilizotolewa na kampuni 
ya Vodacom leo ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona 
visiwani humo, ambapo walifanya makabidhiano kwa njia ya mtandao. 
Pembeni ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia. 
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali
 Iddi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shaaban Seif 
Mohammed wanaonekana kwenye Skrini wakiongea na Mkurugenzi Mkuu wa 
Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania 
Foundation, Rosalynn Mworia wakati Taasisi ya  Vodacom Tanzania 
Foundation walipokabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa serikali ya 
Mapinduzi Zanzibar leo ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya
 Corona visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao


 




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...