Na Shukrani Kawogo, Njombe

Kutokana na kuenea kwa ungonjwa wa COVID 19 Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kimetoa msaada wa barakoa elfu moja kwa wafanyabiashara ndogondogo pamoja na vituo vya bodaboda vilivyopo maeneo ya mjini.

Akizungumza katika zoezi hilo la ugawaji Mwenyekiti wa vijana wa chama hicho ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa na wilaya Theopista Mhagama amesema kuwa wameamua kugawa barakoa hizo katika makundi hayo kwakuwa yanamuingiliano mkubwa wa watu ambapo wanatarajia kuendelea na zoezi hili katika maeneo mengine.

Alisema wameagiza barakoa nyingine zaidi ya elfu tatu ambazo watazigawa katika maeneo mbalimbali yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.

“Tumejipanga kuwasaidia watu mbalimbali hasa wale wanaofanya shughuli zao katika maeneo yenye mikusanyiko ya watukwa kuwagawia barakoa ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona”, Alisema Theopista.

Aidha kwa upande wa katibu wa umoja wa wanawake wa chama hicho wilayani humo Flora Kapalia amesema kuwa barakoa hizo wamezigawa katika vituo vitano vya bodaboda, soko la mbogamboga, soko la samaki na soko la matunda.

Alisema wameamua kufanya zoezi hilo ili kuhakikisha wananchi wao wanakuwa salama na wanajilinda vyema juu ya gonjwa hili.

Hata hivyo kwa upande wa wafanya biashara hao pamoja na waendesha bodada wamelipokea vizuri zoezi hilo na wamekishukuru chama hicho kwa kuwajali.

Naye Katibu wa vijana wa bodaboda Ludewa mjini Jacob Haule amesema kuwa watu wamekuwa wakilipuuza gonjwa hili kitu ambacho ni hatari kwa maisha yao hivyo kwa kuwagawia barakoa hizo zitasaidia kuhamasisha watu kujikinga na kuchukua tahadhari zaidi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...