Na Ahmed Mahmoud, Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk, Hamis Kingwangalla amesema kuwa hatuwezi kushuhudia  sekta ya utalii ikipigwa na janga la Covid - 19 wakati kunamianya mbalimbali ya kuifungua sekta hiyo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayopaswa kuchukuliwa ili watalii waje nchini.

Dk, Kingwangalla aliyasema hayo jana Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini katika maandalizi ya mpango wa kupokea watalii baada ya janga la Covid - 19.

Alisema sekta ya utalii itakuwa ni sekta ya kwanza kaamka hivyo kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea na ikumbuke sekta hii ni sekta nyeti inayoingiza fedha nyingi za kigeni.

Alisema ni vyema sasa tujadiliane jinsi ya kuweka mambo mbalimbali ili kuifungua sekta ya utalii ingawa si jambo rahisi maana sekta hii imeathirika sana na ugonjwa huu hivyo lazima tujadili ili kuweka mikakati ya kuweka mbele yetu na baadaye tufungue milango ya kibiashara
"Tunakila sababu ya kujenga imani katika soko hili la utalii ikiwemo upimaji wa Corona kwa wageni wetu na jinsi ya kudhibiti sababu hatutaki tumwambukize virusi mtalii na sisi tusiambukizane"

Lazima tuangalie msingi ya afya iliyotolewa na inayotolewa na sekta za afya tuonaona nchi mbalimbali zimeanza kufungua mipaka yake na sisi lazima tuwe na viwango vibavyitakiwa ili kuwahudumia watalii wataokutwa na virusi tutawahudumiaje

Alisisitiza ugonjwa huu upo hivyo ni lazima sasa kutafuta mbinu zaukuhakikisha  tahadhari  mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwemo kuhakikisha tunajaribu kufanya utalii kwa tahadhari kubwa na kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wizara husika.

"Haya tutakqyoyajadili lazima tuweke imani na kufuata muongozo itakayokubaliwa na serikali ikiwemo kuweka viwango vinavyotakiwa hivyo ni lazima tujadili jambo hili kwa kina na kisha kesho (jumanne) nitaongea kwa kina na vyombo vya habari ili kusema yale tuliyokubaliana "

Sekta hii imeathirika sana kwa familia zinazotegemea utalii sekta binafsi, mahoteli na sehemu nyingine hivyo lazima tujadiliane na kuyafikisha katika mamlaka zinazohusika.Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Profesa Adolf Mkenda alisema kikao hicho ni muhimu na ni lazima watu wawe wazalendo katika kuhakikisha sekta ya utalii inanyanyuka tena

Kikao hicho kinashirikisha washiriki kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania  (Tanapa) , Mamlaka ya Hifadhi ya Njiro (NCAA) , Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori  Tanzania (Tawa)  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Uhamiaji.
 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk, Hamis Kingwangalla

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...