Na Amiri kilagalila,Michuzi TV-Njombe


Ikiwa Siku chache zimepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,John Pombe Magufuli kufungua milango kwa watafiti wakiwemo wataalamu wa tiba asilia kufanya uchunguzi ili kubaini dawa ya kutibu ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19),hatimae huko mkoani Njombe mtu mmoja ambaye ni mtaalamu wa tiba asilia na tiba mbadala anaefahamika kwa jina la Ally Mhagama maarufu Dr Sagasaga amekiri kufanya utafiti na kuvumbua dawa ambayo anadhani inaweza kutibu ugonjwa huo.

Akitoa agizo hilo alipoketi na vyombo vya ulinzi na usalama hivi karibuni wilayani Chato Rais Magufuli aliwaomba watanzania kutumia njia mbalimbali za asili katika kupambana na Corona.

“Lakini niwaomba waTanzania tujitahidi kutumia njia nyingine za asili katika kupambana na magonjwa haya”alisema Rais Magufuli

Dr Sagasaga ni mtaalamu wa tiba asili na tiba mbadala kutoka kijiji cha Nundu halmashauri ya mji wa Njombe, anasema kilichomsukuma kufanya utafiti na kufanikiwa kufikia hatua hiyo ni Malaika na kwamba ilimchukua muda mwingi porini kuisaka miti ya dawa na kuichanganya ili kupata dawa au kinga ya virusi vya Corona

“ Kwa hiyo nilivyombiwa na Malaika wangu kwenda kutafuta dawa kwa ajili ya kukabiliana na Tatizo nikaona kama haiwezekani laikini nilienda kuchukuwa dawa mara ya kwanza kwasababu zingine zinatoka Mbinga na nyingine maeneo haya,sasa namna ya kutengeneza niliambiwa namna ya kugawanya ndio maana hapa nina makundi matatu”alisema Dkt,Saga Saga

Aidha Saga Saga anasema amefanikiwa kutoa maelezo kwa serikali ya mkoa wa Njombe kutoka hatua ya kwanza lakini bado viongozi hawajafanikwa kumfikia kutokana na majukumu Mengine.

“Nilimtafuta mkuu wa mkoa akaniambia nimemshirikisha mganga mkuu kwa hiyo tutakuja kuona kitaalamu tunafanyaje,name nikamwambia natoa dawa zangu mpeleke Maabara kwa mkemia mkuu na kama dawa hii itatoa majibu mazuri ahadi yangu nitaikabidhi serikali ujuzi wangu ili ione namna ya kuwahudumia wananchi”

Na hapa anafafanua matumizi ya dawa hiyo

“Kuna mimea jumla sita ninayoitumiwa ikiwemo tangawizi na mwarobaini na kuna miti mingine siwezi nikasema,Lakini dawa hii matumizi yake unaivuta huku nyingine unakunywa kidogo na kuiacha kwenye koo kwa muda na kuikoromea,unasafisha koo ni chungu kidogo kama kuna wadudu watoka”alieleza jinsi inavyotibu

Katika hatua nyingine Saga Saga ameiomba serikali kuifanyia uchunguzi dawa hiyo kama ilivyo kwa dawa iliyochukuwa Madagaska kwa kuwa anaamini na dawa aliyoitengeneza kwa mimea ya hapa nchini.

Naye kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Devid Ntahindwa amesema mpaka sasa ofisi yake haijapata Mganga aliyejitokeza na dawa inayoweza kutibu Corona huku akiomba wajitokeze ili kushirikiana katika chunguzi.

“Kuna njia ya kuthibitisha kama hiyo dawa inaweza ikatibu lakini mpaka sasa hatujapata Mganga aliyejitokeza kwamba ana dawa inaweza kutibu Corona na tunatoa rai watumie nafasi hii kutushirikisha na sisi katika chunguzi zao ili kufanya dawa zao ziwe rasmi”alisema Ntahindwa

Hata hivyo licha ya mtaalamu huyo kujitokeza hadharani na kuonyesha dawa aliyoweza kuitengeneza,wapo wengine akiwemo Mbunge wa Lushoto Shabani Shekilindi akihojiwa na kituo cha radio cha East Africa radio,amedai amegundua dawa inayotibu ugonjwa wa Corona, ambapo kwa sasa ameikabidhisha serikalini ili kupata uthibitisho wa Maabara. Shekilindi ameeleza mpaka sasa ameshatibia wagonjwa zaidi ya 30 na wote wamepona.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama nae katika mtandao wa Twita wa Darmpya blog amenukuliwa kueleza kuwaibua vijana waliotengengeneza dawa ya kukinga Corona na kutibu Corona.

"Nimefanikiwa kuwaibua Vijana waliotengeneza dawa inayokinga na kutibu corona (Baycaro kiboko ya corona) ambayo tayari imepelekwa NIMR ili ifanyiwe utafiti.Tunayo pia dawa ya kujifukiza na viwanda vya mask" Assumpter Mshama,DC Kibaha katika nukuu ya mtandao wa twita wa Darmpya blog

Aidha waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kwa niaba ya Tanzania Mei 8, 2020 alipokea msaada wa dawa zinazofubaza Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 kutoka Serikali ya Madagascar,huku akibainisha kufanyiwa uchunguzi kabla ya matumizi.

Mnamo Mei 3, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa atatuma ndege Madagascar kwenda kufuata dawa ya hiyo ya mitishamba. “Nimewasiliana na Madagascar kuna dawa ya corona wameipata nitatuma ndege hiyo dawa ije hapa,” alisema Magufuli.

Nao Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu Corona kufanyiwa majaribio kwanza na kuonya kuwa huenda watu wakaona wamepata tiba na kujihisi kuwa salama ikiwa watakuwa na imani na dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio.
 Mtaalamu wa tiba asili na tiba Mbadala Ally Mhagama maarufu Dkt Saga Saga kutoka kijiji cha Nundu mkoani Njombe akiwa ameshika dawa anayodai inatibu Corona.
 Dkt Saga Saga akionyesha aina ya dawa zake alizoandaa kwa ajili ya kutubu Corona.
 
 Dawa zinazodaiwa kutibu Corona zinazotengenezwa na mtaalam Dkt,Saga Saga kutoka Nundu mkoani Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...