Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akishauri namna ya kuboroa mfumo wa
mawasiliano wa Taasisi hiyo kidijitali.
Na Sixmund J.Begashe Makumbusho
ya Taifa nchini imeweka mikakati ya kuimarisha mifumo ya kimawasiliano kidijiitali
ili kuendana na kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.
Akizungumza
katika kikao maalumu cha kupitia hatua za Maboresho ya Mifumo hiyo kilicho
udhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya uongozi wa Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mkuu
wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema ni wakati sasa wa kuhakikisha
Makumbusho inatumia njia rafiki na zenye kuvutia katika kuifanya Taasisi
iwasiliane na umma.
“Mifumo hii ikiboreshwa itasaidia sana watu
mbali mbali wa ndani na nje ya nchi kupata taarifa za huduma zetu kwa haraka
zaidi, kupokea taarifa kutoka kwenye vyanzo mbali mbali, pia licha Taasisi
yetu kuonekana ya kisasa zaidi, mapato yetu yataongezeka”
Aliongea Dkt Lwoga
Akielezea
hatua mbali mbali zilizo fikiwa katika Maboresho hayo, Mkuu wa kitengo cha
TEHAMA Bw Lusekelo Kaisi alisema kuwa
muda si mrefu Tovuti ya Taasisi itakuwa na mwonekano mpya na yenye taarifa
nyingi na zenye kuvutia.
“Kitengo cha TEHAMA kimejizatiti kuhakikisha
vikao vinaendeshwa kidijitali kama njia ya mapambano ya homa kali ya Mapafu
inayo sababishwa na Virusi vya KORONA na pia kuipunguzia Taasisi gharama”.
Alisema Bw Kaisi.
Kikao
hicho kilicho fanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kilihusu
maboresho ya Tovuti ya Shirika, uwendeshaji wa vikao vya kiofisi, ukusanyaji wa
taarifa kutoka katika vituo vya Makumbusho nchini na kutoka kwa vyanzo mbalimbali
nje ya Makumbusho za Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...