Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Ngao za Uso ‘ Face Shields’ 60 zenye thamani ya shilingi 240,000/= kwa ajili ya watoa huduma za afya katika vituo vyote mkoani Shinyanga vilivyotengwa kwa ajili ya kuhudumia watu waenye maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mhe. Azza amekabidhi Ngao hizo za uso leo Ijumaa Mei 8,2020 wakati akikabidhi gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto katika Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Ngao hizi za uso zikasaidie watoa huduma za afya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona katika maeneo/vituo vilivyotengwa mkoani Shinyanga kuhudumia wagonjwa wa Corona”,alisema Mhe. Azza.

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kusambaza taarifa za uongo kuhusu Corona kwenye mitandao ya kijamii.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko Ngao za Uso ‘ Face Shields’ 60 zenye thamani ya shilingi 240,000/= alizotoa kwa ajili ya watoa huduma za afya katika vituo vyote mkoani Shinyanga vilivyotengwa kwa ajili ya kuhudumia watu waenye maambukizi ya Virusi vya Corona. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dkt. Fidelis Mushi (katikati) Ngao za Uso ‘ Face Shields’ 60 zenye thamani ya shilingi 240,000/= alizotoa kwa ajili ya watoa huduma za afya katika vituo vyote mkoani Shinyanga vilivyotengwa kwa ajili ya kuhudumia watu waenye maambukizi ya Virusi vya Corona. 
Mganga Mfawidhi kituo cha afya Tinde Dkt. Greyson Matogo (katikati) akiwa amevaa Ngao ya uso 'Face Shield' ambayo ni sehemu ya Ngao zilizotolewa na Mbunge Azza Hilal.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...