Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani( katikati) akizungumza na mwanakijiji wa Izunya,( kushoto) ambacho kikokaribu na miundombinu ya umeme ambapo aliigiza TANESCO, kupeleka umeme katika vijiji vya aina hii ambavyo vimepitia au vipo karibu na miundombinu ya umeme ambavyo havijafikiwa na REA, alipofanya fanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita.
Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani ( kushoto) akizungumza katika kituo cha afya cha Nyang’hwale alipofika kuwasha umeme katika zahanati hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita
Kituo cha afya cha nyang’hwale kilichowashiwa umeme na Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita
Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani( kulia) akikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Buseresere na kuiagiza TANESCO, kupeleka umeme katika zahanati hiyo ili kurahisisha na kuharakisha ujenzi wa kituo hicho, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita
Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani(kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa ofisi ndogo ya TANESCO,Katoro baada ya kutoridhishwa na mpangilio wa ofisi, mahudhurio na utendaji kazi wa watumishi wa kituo hicho, na kumuagiza meneja huyo kuandika barua ya kujieleza juu ya mapungufu hayo kabla ya kuchukuliwa hatua, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hiyo, wakati ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijiji katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita.
Meneja wa Ofisi Ndogo ya TANESCO, Katoro akifungua mlango katika moja ya ofisi za watumishi,iliyokuwa imefungwa saa za kazi baada ya kuagizwa na Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani( pili kushoto)alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita.
Miundimbinu ya umeme( kulia) ikionekana imekoma jirani na kijiji cha ambacho bado hakijafikiwa na mradi wa REA,Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani aliigiza TANESCO, kupeleka umeme katika vijiji vya aina hii, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita.
Muonekanao wa miundombinu ya umeme inayopita katika baadhi ya vijiji mbacho havina umeme ama vipo jirani na miundombinu ya umeme na hakijafikiwa na Mradi wa REA, Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani aliigiza TANESCO, kupeleka umeme katika vijiji vya aina hii, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita


Na Zuena Msuya, Geita

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) watakaoshindwa kutimiza malengo ya kuunganisha umeme vijijini na kuwawashia wananchi umeme watachukuliwa hatua kwa mujibu wa mikakati iliyowekwa katika kupima utendaji kazi wao.

Dkt. Kalemani alisema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea baadhi ya vijiji ambavyo vimepitiwa na vilivyojirani na miundombinu ya umeme ambavyo bado havijafikiwa na mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA katika Wilaya ya Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita, Mei 15, 2020.

Baada ya kukagua vijiji hivyo aliwaagiza Mameneja wa TANESCO nchini kuunganisha umeme katika vijiji hivyo pamoja na kuwawashia wananchi umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 tu.

Dkt. Kalemani aliweka wazi kuwa katika kutimiza azma na malengo ya serikali ya kuhakikisha kuwa vijiji vyote nchini vinapata umeme, mameneja wa TANESCO kote nchini waliwekewa vigezo vitatu vya kuwapima na kufanya tathmini ya utendaji kazi wao katika kutekeleza malengo hayo, zoezi hilo lilianza mwezi Julai, 2019, ambapo sasa utekelezaji wake unaanza kwa kuwachukulia hatua mameneja hao.

Vilevile mameneja walitakiwa kuunganisha umeme katika vijiji ambavyo vimepitiwa na njia ya kusafirisha umeme mkubwa ambavyo bado havijafikiwa na REA pamoja na vile vilivyo umbali mfupi kutoka katika maeneo yaliyopitiwa na njia za umeme.

Alitaja tathmini zinazotumika kuwapima mameneja katika utendaji kazi wao, kuwa ni kuongeza idadi ya wateja katika maeneo yao na kuunganisha wateja hao kwa wakati mara tu baada ya mteja kulipia gharama za uunganishaji, tathmini hiyo inachukuwa 45% ya utendaji kazi wake.

Aidha Mameneja hutathminiwa kwa kutoa huduma bora kwa wateja, hii inatokana na baadhi ya mameneja kutokuwa na ushirikiano na wateja katika maeneo yao, pia kutokupokea simu za wateja wala wa kusikiliza kero na kutatua changamoto zao, hii inachukuwa 20% na Tatu ni kukatika kwa umeme mara kwa mara bila sababu wala kutoa taarifa kwa wateja katika eneo lake ambalo huchukuwa 30% ya tahmini yake.

“Kama unakataa wateja katika eneo lako, umeme unakatika mara kumi kwa mwezi, huwasikilizi wateja wala kutatua kero zao,hupokei simu za wateja wewe hutoshi na hufai kuwa maneja andika barua ujitoe mwenyewe, pia tunakutoa, mameneja wa kanda simamieni hili na muanze kuchukuwa hatua, na kama hamtachukuwa hatua tutaanza kuwatoa kuanzia chini mpaka juu” alisisitiza Dkt. Kalemani.

Aidha alifanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi Ndogo ya TANESCO ya Katoro na kumtaka meneja wa kituo hicho kuandika barua ya kujieleza, kutokana na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo kutokuwepo kazini bila taarifa yoyote, na wengine kukutwa wakipiga soga bila kuwepo katika maeneo yao ya kazi.

Vilevile ofisi hiyo haikuwa alama au vibao vinavyomuelekeza mteja katika dirisha husika la kutolea huduma kama vile eneo la mapokezi, mhasibu na meneja wa kituo.

Kuafuatia hali hiyo alizataka ofisi za TANESCO nchi kote kuendeshwa kwa kuzingatia nidhamu za kazi,pia watendaji waache kufanya kazi kwa mazoea kwa lengo la kutoa huduma bora wateja.

“Hii ni ofisi ya TANESCO kweli!hakuna alama inayoonyesha sehemu ya mapokezi, kwa mhasibu wala meneja, nimekuja hapa mpaka naingia ndani hakuna hata wa kunipokea, sasa mimi ni Waziri, je akija mwananzengo( mwananchi) atapata huduma kweli! Waliopo ofisi wale kule wanapiga soka wanaacha kukaa sehemu zao kazi!mchora michoro yuko wapi na wengine je! Meneja unaendesha ofisi kwa mazoea eee nataka maelezo la sivyo….!”, alifoka Dkt. Kalemani.

Akiwa katika Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Kalemani aliwasha umeme katika kituo cha afya katika eneo hilo, kukagua usambazaji wa umeme katika kijiji cha Izunya na na kuwagiza TANESCO kupelekea umeme katika vijiji hivyo ambavyo vipo karibu na miundombinu ya umeme na havijafikiwa na mradi wa REA kwa awamu zilizotngulia.

Katika Wilaya ya Geita aliagiza kuunganisha umeme katika kijiji cha Shinamwendwa kilichopitiwa na njia ya kusafirisha umeme mkubwa na kijiji cha Chibingo ambavyo vyote hakijafikiwa na mradi wa REA, na katika wilaya ya Chato aliwasha umeme katika moja ya kanisa katika kijiji cha Buzirayombo na kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Buseresere na kuagiza TANESCO kupeleka umeme katika kituo hicho ili kuharakisha ujenzi wa kituo hicho.

Katika hatua nyingine alimtaka mkandarasi anayetekeleza usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya ya Nyang’hwale kukamisha kazi ya kuwasha vijiji vilivyosalia na akishindwa kufanya hivyo atakatwa 10% ya malipo yake na kuchukulia hatua za kisheria kwa kuchelewesha huduma kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...