Na Ripota Wetu,Michuzi TV
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa John Kabudi amesema amepokea kwa masikitiko makubwa ,majonzi na mfadhahiko mkubwa taarifa za kufariki Dunia kwa Balozi Dk.Agustine Mahiga huku akieleza kuwa Tanzania imempoteza mwana halisi wa Tanzania na mzalendo aliyeitumikia nchi kwa moyo na akili zake zote.
Balozi Dk.Mahiga amefariki Dunia leo Mei 1, mwaka 2020 na kifo chake kimeishtua Mataifa mbalimbali kutokana na mchango wake mkubwa kwenye eneo la diplomasia ambalo Balozi Mahiga alibobea na kutoa mchango mkubwa kwa Mataifa mbalimbali.
Akizungumza leo kuhusu kifo cha Balozi Dk.Mahiga, Profesa Kabudi amesema kwamba ni pigo kubwa na kifo hicho amekipokea kwa masikitiko makubwa na majonzi taarifa za kufariki dunia kwa Balozi Dk.Aguastine Mahiga aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria .
Profesa Kabudi amefafanua kabla ya hapo kutoka mwaka 2015 hadi Machi2019 Dk.Mahiga alikuwa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki aliyemuachia kijiti .
"Dk.Mahiga ambaye namfahamu kama mwalimu mahiri kwenye miaka ya 1970 tena akiwa kijana mwenye bashasha,mchangamfu na mwenye umahiri mkubwa wa kuzungumza lugha ya Kingereza na fundi katika kujieleza, baadae akawa mtu mashuhuri ,Mwanadiplomasia aliyebobea.
"Alikuwa mtu muungwana, mtu mwema,mwadilifu ,mzalendo kwa nchi yake ambaye ametumikia nafasi na nyanja mbalimbali. Katika kipindi chake cha Uwaziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki ,mimi nikiwa Waziri wa Katiba na Sheria, nimepata bahati ya kutumwa na Rais Dk.John Magufuli kumsindikiza Balozi Mahiga katika baadhi ya shughuli zake mbalimbali,"amesema Profesa.Kabudi.
Ameongeza kuwa katika kutumwa huko amejifunza nimejifunza mambo makubwa sana ya umahiri,ustadi, ufundi,udhabiti wa Balozi Mzee Dk.Mahiga katika kuyatetea maslahi ya Tanzania ,kuitetea Tanzania lakini pia katika kujenga madaraja mazuri ya uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali.
"Mimi binafsi natoa rambirambi nyingi kwa familia yake ,kwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msiba huu mkubwa uliotupata.Tuyaenzi yale yote ambayo Balozi Dk.Mahiga aliyoyafanya enzi za uhai wake na moja tujifunze kwake utiii usiotetereka ,unyenyekevu uliomithirika lakini zaidi kubwa zaidi uzalendo wake katika kusimamia nchi yetu.
"Mzee Dk.Mahiga amefanya kazi kubwa akiwa kwenye utumishi wa Serikali ya Tanzania, utumishi wa Umoja wa Mataifa na akiwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa kusuluhisha mgogoro wa Somalia uliowezesha nchi hiyo kupata Serikali ya awali, kwa hiyo tunaweza kuona sote mchango wa Balozi Mahiga haukuwa Tanzania tu,haukuwa Afrika tu bali ulitambulika katika ngazi katika za Kimataifa alipokuwa akifanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi,"amesem Profesa Kabudi.
Pia amesema Balozi Dk.Mahiga alitambulika kwenye medani ya Kimataifa alipokuwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na kwamba kweli Tanznaia imepoteza mwana halisi wa Tanzania na mzalendo aliyeitumikia nchi yake kwa moyo wake wote,nguvu zake na akili zake zote kwa ujasiri na uaminifu mkubwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...