
Mratibu wa mtandao Habari za jamii za pembezoni(MAIPAC) Mussa Juma akiwa na Mkurugenzi wa taasisi ya CILAO, Odero Charles wakimkabidhi mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa Arusha,Claude Gwandu vifaa kinga dhidi ya Corona kwa waandishi wa habari lakini pia muongozo wa kufanyakazi kwa tahadhari kwa vyombo vya habari.
Na Vero Ignatus Arusha.
Waandishi wa habari mkoa wa Arusha, wametakiwa kuongeza tahadhari za kiafya katika kujikinga na maambukizi ya Covid -19 kwa kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu wa afya kwani Maisha yao thamani zaidi ya habari.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama Cha waandishi mkoa wa Arusha, Claud Gwandu wakati akipokea msaada wa vifaa kinga na muongozo wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kutoka mtandao wa waandishi wa habari za jamii za pembezoni(MAIPAC) na Asasi
za CILAO na PINGOs forums.
Gwandu alisema wanahabari ni lazima watambuwe hakuna habari ambayo inathamani zaidi ya maisha yao, hivyo ni muhimu kuchukuwa tahadhari zote kwa kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kufuata miongozo ya serikali.
Mkurugenzi wa shirika la CILAO, Odero Charles alisema wametoa msaada huo wa pamoja ili kusaidia wanahabari mkoa wa Arusha na manyara kupambana na maambukizi ya Corona.
Alisema ni muhimu wanahabari na vyombo vya habari mkoa wa Arusha na Manyara, kufuata muongozo wa kufanya kazi kipindi hiki hasa kwa kujitahidi kutokwenda bila tahadhari maeneo ya mikusanyiko, kutofanya mahojiano ya ana kwa ama na vitendea kazi kuvisafisha mara kwa mara.
Mkurugenzi wa shirika la PINGOs Forum, Edward Poroka alisema sambamba na kusaidia wanahabari kupitia taasisi za MAIPAC na CILAO pia wametoa msaada kwa halmashauri ya Simanjiro na Longido wa vifaa vya kupambana na Corona vyenye thamani za zaidi ya sh 25 milioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...