Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea
kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria,
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) kilichotokea leo alfajiri Mei 01,
2020 Jijini Dodoma.
Tume inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na
kiongozi mchapakazi, mwadilifu, mzalendo
na mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja
za Kimataifa kwa miaka mingi.
Aidha, Tume inatoa
salamu za pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job
Yustino Ndugai, Wabunge, Wafanyakazi wa Wizara
ya Katiba na Sheria, familia ya Marehemu na wananchi wa Mkoa wa Iringa
kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Tume ikiwa taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na
Sheria inaungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu na inawaomba
wanafamilia wote kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala
pema peponi, Amina.
Imetolewa na:
Jaji (Mst) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu
Mwenyekiti
TUME
YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Mei 01, 2020
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...