Na Woinde Shizza , KILIMANJARO
DIWANI wa Kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro Juma Raibu amekabidhi barakoa 100,vitakasa mikono pamoja na ndoo kwa wafanyabiashara wa Soko la Pasua ili kujikinga na virusi vya Corona ambavyo vinaendelea kutikisa Dunia.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Diwani huyo amesema kuwa ameamua kutoa vifaa vya kujikinga na Corona kwa wananchi hao ,ili kuendelea kuchukuwa taathari
Amesemambali na kutoa vifaa hivyo pia ametoa elimu ya kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona 19 kwa wananchi wa Kata ya Bomambuzi pamoja na wafanyabiashara wa masokoni ya Pasua pamoja Mbuyuni huku alibainisha kuwa wataendelea kutoa vifaa vyakujikinga na elimu kwa kila mwananchi.
Aidha amewaomba wananchi hao kufata maelekezo ya wataalamu wa afya na maagizo ya Serikali huku wakizingatia zaidi kuepuka misongamano isiyo ya lazima.
Pia Diwani huyo amewaonya wananchi wanaopotosha jamii kuhusu idadi ya wagonjwa pamoja na wanafariki kwa virusi vya Corona na kusema kuwa iwapo atabainika mtu anafanya hivyo hatua Kali zitachukuliwa thidi yake, huku akiliagiza jeshi polisi kuwachukulia hatua kali za kisheriavifaa hivyo .
amesema wamehamasisha jamii juu ya kuweka na kunawa na maji tiririka na sabuni kwenye sehemu zote za biashara nyumbani na maeneo yote yenye mikusanyiko, wametoa elimu kwenye masoko.
Akitoa shukrani kutokana na msaada huo mmoja wa wafanya biashara wa soko la Pasua Gloria Mboya ameema kuwa anashukuru kwa diwani huyo kwa kuendelea kuwajali wananchi wake kwa kuwapa vifaa vya kujikinga pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kuendelea kuchukuwa tahathari ya ugonjwa huo.
Ameseema kuwa ugonjwa huo upo hivyo ni vyema kila mtanzania kuendelea kujikinga na kufuata maelezo yanayotolewa na wataalam,huku akikisitiza kuwa iwapo mtu yeyote akijihisi anadalili za ugonjwa huo kuwa maramoja hospital kwa ajili ya kupata huduma.
Diwani wa kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa Ya Moshi Juma Raibu akiendelea kuwafundisha wananchi namna ya kuvaa barakoa(picha na Woinde Shizza, Kilimanjaro).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...