Na Abdullatif  Yunus Michuzi Tv.

Taasisi ya Umoja wa Maendeleo ya Wanawake wa Kiislamu Kagera (UMWAKIKA) yenye Makao makuu Manispaa ya Bukoba wametumia Siku ya Mama Duniani kuhamasisha Jamii kwa ujumla kuendelea kujitokeza kuchangia michango ya hali na Mali katika Ujenzi wa Kituo cha Afya kinachoendelea kujengwa Katika Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.

Wazo la Ujenzi wa Kituo hicho lilianzishwa na akina mama hao mnamo mwaka 2012,  lengo likiwa ni kuendelea kurahisisha huduma za afya hasa Kwa Mama na Mtoto, licha ya kuwa Ujenzi huo umekuwa ukisuasua kutokana na uwezeshwaji wa vifaa vya Ujenzi pamoja na Fedha za kuendeleza mradi huo, huku akina mama hawa wakitegemea sadaka na michango ya wahisani.

Mpaka sasa ikiwa ni miaka minane ya Ujenzi wa Kituo hicho hakuna jengo lililokamilika kati ya majengo Saba yanayofikiriwa kujengwa hapo, juhudi zikiwa bado katika jengo moja linaounganisha wodi ya kulaza wagonjwa, chumba cha daktari, stoo na chumba cha dawa, jengo likiwa katika hatua ya ukamilishwaji.

Akizungumza kuhusu Kituo hicho mara baada ya shughuli ya usafi wa kituo hicho, Kiongozi wa Taasisi hiyo Bi. Rabiat Byamungu mbali na shukrani zake kwa wadau mbalimbali waliowasidia kwa namna mbalimbali, amesema kwa miaka yote hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya akina baba, wameweza kuendesha Harambee na  makongamano mbalimbali yakiwemo ya Dini, lengo likiwa ni kupata michango, na hivyo kupitia michango na sadaka hizo ndiyo sababu ya Jengo hilo kufikia hapo lilipofikia, "Tunaomba wadau mzidi kutushika mkono, nguvu zetu ni ndogo, tunazunguka na bahasha zetu kutafuta michango, nguvu zetu ni kidogo akina mama mnatujua, tumeona tuwambie wadau wetu" amesema Bi. Rabiat.

Ili kuchangia Ujenzi huo, unaweza kuchangia vifaa vya Ujenzi au pesa taslimu kwa  kuwasiliana na Viongozi wa Taasisi hiyo kwa Namba 0754896704 (Katibu), au 0713958202 (Mwenyekiti), au unaweza kutuma mchango wako Benki ya NBC akaunti namba 027206011123 Jina ni Umoja wa Maendeleo ya Wanawake.
 Pichani ni Muonekano wa Jengo mojawapo kati ya Majengo saba ya Kituo cha Afya ambacho kinasimamiwa na Taasisi ya UMWAKIKA
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...