Ofisa Miradi wa Can Tanzania Jophillene Bejamula akizungumza mbele ya wawakilishi wa asasi mbalimbali ambazo zimejikita kwenye sekta ya nishati jadidifu na mazingira wakati wa mkutano wa kujadili na kuweka mikakati ya kuendelea kuielimisha jamii kuhusu kutumia nishati hiyo
Mkuu wa Programu kutoka Can Tanzania Boniventure Mchomvu(aliyeinama) akiandaa mada kwenye kompyuta mpakato kwa ajili ya kutolewa kwa washiriki walioshiriki mkutano ambao umewakutanisha wadau wa sekta ya nishati jadidifu.
Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ,Bwawani Chalinze Kazi Ramadhan akiwa makini kusoma maelezo yanayohusu nishati jadidifu wakati wa mkutano uliowkautanisha wadau waliojikita kwenye sekta ya nishati jadidifu na mazingira.
Mkuu wa Mafunzo na Maendeleo ya Biashara Daniel Mwingira kutoka Kampuni ya Nukta Africa akifafanua jambo mbele ya washiriki kuhusu njia rahisi ya kutumia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu masuala ya nishati jadidifu.
Mkuu wa Programu kutoka Can Tanzania Boniventure Mchomvu akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.

Mmoja ya washiriki akielezea namna ambavyo asasi za kiria zinavyoweza kushirikiana kuhamasisha jamii kutumia nishati jadidifu ambayo ni rafiki mkubwa wa mazingira.
Joseph Mista kutoka Kampuni ya Sepon Ltd akichangia jambo wakati wa mkutano huo uliwaowakutanisha wadau wa sekta ya nishati jadidifu na mazingira.
Mmoja ya washiriki akifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo ukiendelea.

Ofisa Miradi wa Can Tanzania Jophillene Bejamula akiendelea kuandika hoja za washiriki wa mkutano uliwaokutanisha wadau kujadili na kuweka mbinu za kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia nishati jadidifu pamoja na kuelezea miradi ambayo imetekelezwa
Deus Kagenzi kutoka asasi ya Tayen akieleza jambo mbele ya washiriki wa mkutano huo







Na Said Mwishehe, Michuzi TV

ASASI ya CAN Tanzania imezishauri asasi za kiraia kuendelea kushirikiana katika kutoa elimu na kuwezesha upatikanaji wa mali fedha ili kusaidia miradi ya kuhamasisha na kukubalika kwa nishati safi pamoja na nishati jadidifu.

Hayo yamesemwa na Ofisa Miradi Can Tanzania Jophillene Bejamula wakati wa majadiliano yalishorikisha wadau wa mazingira kutoka asasi za kiraia zilizokutana kujadili na kubadilisha mawazo kuhusu mbinu sahihi zitakazosaidia kuhamasisha jamii kutumia nishati jadidifu.

"Asasi ziendelee kushirikiana katika kutoa elimu na kuwezesha upatikanaji wa mali fedha ili kusaidia miradi ya kuhamasisha na kukubalika kwa nishati safi,"amesisitiza.

Hata hivyo amesema kuwa Wizara ya Nishati, Serikali za Mitaa pamoja na asasi za kiraia ziko mstari wa mbele katika kuendeleza nishati safi.

Akizungumzia Can Tanzania, amesema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwezesha matumizi ya nishati safi katika maeneo ya kijiji cha Kidomole na Kata ya Makurunge ndani ya Wilaya ya bagamoyo.

"Kata ya Makurunge na kijiji cha Kidomole wametengeneza na wameanzisha kutumia mpango mkakati wa vijiji katika kuboresha na kutumia nishati safi,"amesema.

Kuhusu changamoto amesema kubwa hasa ilikuwa watu na wadau wengi walitamani kushiriki kupewa elimu na ushirikiano katika kubaini majiko banifu lakini kutokana na bajeti ndogo, hivyo waliweza kufikia wananchi, wafanyakazi na viongozi wa vijiji wachache.

"Katika kufanikisha mradi wa nishati jadidifu katika maeneo hayo tumefanikisha wananchi 350 wamepewa elimu , viongozi wa vijiji na kata 32 wamefikiwa na kupewa elimu .Pia maofisa wa Serikali na Ofisa ugani 26 wamefikiwa na kupewa elimu ya nishati safi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao wa mazingira wametumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa jamii kuendelea kupewa elimu na kujengewa uelewa zaidi kuhusu nishati jadidifu.

Wamesema changamoto iliyopo sasa bado kunakosekana msukumo wa pamoja kuhusu matumizi ya nishati safi pamoja na nishati jadidifu, hivyo njia pekee ni kuiwezesha jamii kutambua umuhimu wake kuanzia ngazi ya chini hadi juu.

Joseph Mista kutoka Kampuni ya Sepon Ltd amesema njia mojawapo ya kuhamasisha nishati jadidifu ni kuendelea kuielimisha jamii kutumia nishati jadidifu kuanzia ngazi ya chini.

"Elimu ikiwa na uelewa wa kutosha maana yake huko mbele ya safari hata utashi wa kisiasa utakuwepo,"amesema na kutumia nafasi hiyo kuishukuru Can Tanzania kwa kuwakutanisha wadau hao kujadili miradi ya nishati jadidifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...