
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Jukwaaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuonyesha shukran kwa Zuchu, Manara amesema kuwa kipaji cha msanii huyo ni cha kuvutia sambamba na Msanii Mbosso kwa uwezo wao wanaonesha kumiliki jukwaa kwa mtindo wa 'Live Band' na sauti za kuvutia kwa mashabiki wa muziki.
"Huyu Zuchu amelelewa na Mama Khadija Kopa katika maadili ya dini ya Kiislamu, kaja hapa WCB kiukweli na mimi sina Mke nipo 'Single' naombeni mnipe ridhaa nitamlea katika maadili yaliyo bora", amesema Manara.
Manara pia amewashukuru WCB kwa kuonyesha ushurikiano kwa jamii, Wasanii, pia ametoa pongezi kwa kukuza Wasanii mbalimbali kimuziki.
" Angalia 'Show' ya Mbosso ilivyofana, mimi wakutunza Shilingi Milioni 7 kweli?, kwa hilo hapana Diamond Plutnumz nirudushieni Milioni 3 halafu Milioni 4 chukueni nyie," amedai Manara.
Katika hatua nyingine, Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaasa Wasanii chipukizi kuzingatia zaidi Nidhamu, na Ndoto zao katika kufikia malengo yao baadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...