Shirika
lisilo la kiserikali la Haki Madini limewajengea uwezo wachekechaji 60
wa madini ya Tanzanite wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara juu ya elimu ya afya na usalama.
Afisa
miradi wa shirika la Haki Madini, Emmanuel Mbise akizungumza jana
alisema wachekechaji hao watapatiwa mafunzo hayo kwa muda wa siku
mbili.
Mbise alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanachangia kupunguza athari za afya kwenye shughuli za uchekechaji.
Alisema
pamoja na kutoa mafunzo hayo pia waliwapatia barakoa 400 kwa ajili ya
kujikinga na vumbi wakati wakifanya shughuli zao za uchenjuaji mchanga
wa madini ya Tanzanite.
"Pamoja
na washiriki hao 60 pia kuna viongozi watano wakiwemo wa serikali hivyo
kuwa na washiriki 65 ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa mabalozi
wazuri kwa wengine," alisema Mbise.
Mwenyekiti
wa wachekechaji wanawake wa Naisinyai, Nairukoki Leiyan alisema
mashirika mengine yaige mfano wa Haki Madini katika kuwajali wadau wa
madini ya Tanzanite.
Leiyan alisema mafunzo hayo yatawasaidia kufanya shughuli zao ipasavyo na pia barakoa walizopatiwa zitawakinga na vumbi.
Mmoja
kati ya wachekechaji hao Isaya Maliaki alisema mafunzo hayo
yatawajengea uwezo zaidi wa kufanya kazi zao kwa usalama zaidi tofauti
na awali.
Maliaki
alisema pamoja na mafunzo hayo pia barakoa waliopatiwa zitawakinga na
vumbi wakati wakifanya shughuli zao za uchenjuaji mchanga wa madini ya
Tanzanite.
Alisema
wachekechaji hao wakitekeleza namna walivyofundishwa watakuwa salama
kwani watakuwa wanashika michanga kwa kutumia vikinga mikono wakati
wakifanya kazi zao.
Afisa
afya wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Boniface Jacob aliwapongeza
Haki Madini kwa kuwajengea uwezo wachekechaji hao wa madini ya
Tanzanite.
Jacob alisema
zaidi ya kuwapa mafunzo ya kuwezeshwa kujikinga na vumbi pia barakoa
waliopatiwa zitawakinga na vumbi na maambukizi ya virusi vya corona
kwani wanapaswa kuendelea kujikinga.
Ofisa miradi wa shirika lisilo la kiserikali la Haki
Madini, Emmanuel Mbise akizungumza na wachekechaji wa madini ya
Tanzanite wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwenye
mafunzo ya siku mbili ya elimu ya afya na usalama kwa wachekechaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...