
ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati kuu (CC) ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa NEC, Jerry William Silaa amepata kura 206 huku mtia nia mwezake aliyemfuatia kwa karibu, Robert Masegese akipata kura 118 kwa kupitwa kura 88.
Katika zoezi hilo, jumla ya watia nia 147 walishiriki zoezi hilo, lililoanza mapema leo majira ya saa tatu asububi na kwenda hadi usiku huu.
Jerry Silaa ambaye aliwahi kuwa, Diwani wa Kata ya Gongolamboto na pia Meya wa Ilala alitoa shukrani zake kwa kura alizopata.
Pia Jerry aliwahi kugombea nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo la Ukonga, 2015.
Mwaka 2005 alianza kuwa Diwani katika Kata ya Ukong na baadae 2010 aligombea Udiwani Kata Gongolamboto na wakati huohuo aliweza kuwa Meya wa Ilala.
Jerry alisema 2015 aliamua kugombea Ubunge ili kuleta maendeleo zaidi katika Jimbo la Ukonga hata hivyo hakufanikiwa kupita na kutokukata tamaa na 2020 amemua kurejea tena kutimiza adhima yake hiyo.
Zoezi hilo lilisimamiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Idd Mkowa ambapo alisema zaidi ya wajumbe walioshiriki kupiga kura walikuwa zaidi ya 600.
"Kura 552 zilipigwa huku kura moja ikiharibika na kufanya kura halali kuwa 551."Alisema Mkowa.
Ambapo pia alimtaja Jerry Silaa, kupata kura 206.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...