Na Amiri Kilagalila,Njombe
Tume ya taifa ya
uchaguzi NEC imehitimisha mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo watumishi
126 kutoka mikoa mitatu ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania watakaohusika
katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka
huu.
Akizungumza wakati
wa kufunga mafunzo hayo yalitolewa kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa
,wasimamizi wa uchaguzi,maafisa uchaguzi na Ugavi kutoka mikoa ya Njombe,Ruvuma
na Iringa kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji Mery Langwai amesema
uwezo waliojengewa ukatumike ipasavyo katika kutekeleza majuku yao bila kuvunja
sheria ,taratibu na kanuni za uchaguzi.
“Nina amini
mafanikio katika mafunzo haya yanabashiri uwezo wa kukabiliana na changamoto
zinazoweza kujitokeza katika mafunzo kwa watendaji ngazi ya kata na vitu vya
kupiga kura kadri hatua yautekezaji wa uchaguzi kwa namna nzuri na uelewa mpana”alisema
Jaji Merry Langwai
Katika hatua
nyingine Jaji Langwai ameagiza watumishi hao kwenda kuipeleka elimu hiyo kwa
wasimamizi wa uchaguzi wa uchaguzi ngazi ya kata na vituo ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa weledi katika kipindi chote cha uchaguzi.
“Jukumu lililo
mbele yenu ni kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata na baadaye
mtatoa mafunzo kwa makarani waongozaji,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi
kutoka katika halmashaui zenu”aliongeza Merry Langwai
Baadhi ya washiriki
wa mafunzo hayo akiwemo Iddy Mponda,Lucy Komba na
Hamad Njovu wanasema mafunzo hayo yametolewa katika muda muafaka na kuahidi
kwenda kusimamia zoezi la uchaguzi kwa umakini na kuzingatia misingi na
taratibu ili kupata viongozi bora wa kuwatumikia watanzania katika kipindi
kingine cha miaka 5.
“Mafunzo
tuliyoyapata kwanza yametujengea uelewa wa kutosha hususani kwenye sharia yenyewe
ya uchaguzi lakini pia taratibu zinazotkiwa kufuatwa kuhakikisha uchaguzi
unakuwa wa huru na haki”alisema Iddy Mponda.
Baadhi ya
washiriki wa semina Uchaguzi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kukamilika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri yam ji wa
Njombe
Kamishna wa tume
ya taifa ya uchaguzi jaji Mery Langwai wakati akitoa hotuba ya kufunga mafunzo
ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi katika ukumbi wa halmashauri yam ji wa
Njombe Lunyanywi.
Baadhi ya
washiriki wa semina ya uchaguzi kutoka NEC wakimsikiliza kamishna wa tume ya
taifa ya Uchaguzi wakati akifunga mafunzo ya siku tatu mjini Njombe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...