Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa
ya Matayarisho ya Mazishi ya Marehemu Mzee Bendjamin Mkapa Waziri Mkuu Mh.
Kassim Majaliwa akiwa sambamba na Makamu Mwenyekitiwa Kamati Hiyo Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitoa maelekezo walipofika
Uwanja wa Taifa kuangalia hatua iliyofikiwa ya Matayari ya shughuliza Kuagwa
Mzee Mkapa.Kulia ya Mh. Majaliwa ni Waziri wa Nchi Afisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa anzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na kulia ya Balozi
Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Jenista Muhagama.Picha na – OMPR – ZNZ.
Mafundi wakiendelea na harakati
za kukamilisha matayarisho ya Uwanja wa Taifa kwa ajili ya shughuli za kuuaga
Mwili Wa Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Tatu Marehemu Bendjamin William
Mkapa.
Baadhi ya wapambaji wa maua
wakikamilisha kazi ya upambaji wa jukwa litakalowekwa Mwili wa Mwili Wa Rais
Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Tatu Marehemu Bendjamin William Mkapa aliyefariki
Dunia Usiku wa kuamkia Ijumaa.
======= ======= ========
Matayarisho ya mwisho yanayofanywa na Serikali
katika Uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa
nafasi kwa Viongozi, Wananchi pamoja na Wanadiplomasia kuuaga Mwili wa Marehemu
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Jahumuri ya Muungano wa Tanzanzia Marehemu
Bendjamin William Mkapa yameshafikia hatua za mwisho kukamilika.
Serikali Kuu imeandaa utaratibu huo Maalum ili
kuwapa fursa Wananchi Kuuaga Mwili wa Kiongozi wao hasa ikizingatiwa Utamaduni
na Heshima iliyojengeka kwa Watanzania kutoa Heshima kwa Viongozi wao
waliotangulia mbele ya Haki kuwaaga baada ya kazi kubwa waliyoitekeleza
kulitumikia Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mazishi hayo
Wazirri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Kassim akiambatana na mwenzake Makamu Mwenyekiti Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi walipata fursa ya kukagua Maandalizi hayo na kuridhika na hatua
kubwa iliyofikiwa chini ya Watendaji wa Serikali waliopewa jukumu hilo.
Mwili wa Marehemu Mzee Mkapa aliyefariki Dunia
Ghafla Usiku wa kuamkia Ijumaa utawekwa Uwanjani hapo kuanzia asubuhi ya Kesho
Jumapili hadi Jumanne kwa shughuli hiyo ya kuagwa na Jumatano utapelekwa Kijiji
chake Lupaso Masasi Mkoani Lindi kumalizia ambapo Alhamis Mchana utazikwa rasmi
kwa heshima zote za Kitaifa.
Akizungumza na Watendaji wa matayarisho hayo
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Kitaifa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Kassim
alisema lengo la Marehemu Mzee Mkapa kuzikwa Kijijini kwao nyakati za mchana
limezingatia uhaba wa nyumba za kulala wageni ambapo waomnbolezaji watapa muda
wa kurudi Mikoani mwao mapema.
Mh. Majaliwa alisema Kamati ya itaifa ya Mazishi
imepanga utaratibu kwa kuwawekea muongozo Viongozi wa Kitaifa na wale wa
Kidiplomasia kutoa heshima zao katika uwanja wa Taifa kwa lengo la kupunguza
msongamanop wakati wa mazishi Mkoani Lindi.
Alisema Viongozi wa Mataifa mbali mbali Duniani
wanaendelea kutoa salamu za rambi rambi kwa Tanzania kufutia kifo hicho na
kufafanua kwamba Wale Viongozi wa Kimataifa watakaopata fursa ya kushiriki
tukio hilo watapatiwa kutoa salamu Maalum kwenye shughuli hiyo ya kuuaga Mwili
wa Marehemu.
Naye kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Timu
hiyo iliyopewa jukumu na kufanya matayarisho hayo na kusema kwamba jitihada zao
zimewezesha kufanikisha maandalizi hayo kwa asilimia kubwa.
Balozi Seif alishauri kwamba zile kazi ndogo ndogo
zilizobakia ni vyema kwa wahandisi na watendaji hao wakahakikisha kwamba
zinakamilika kabla ya kufikishwa kwa Mwili wa Marehemu kuanza harakati za
Kuuaga Mwili wake shusghuli zitakazoanza nyakati za asubuhi.
Marehemu Mzee Bendjamin William Mkapa ataendelea
kukubukwa na Watanzania walio wengi hasa kutoka na Falsafa yake ya Ukweli na
Uwazi iliyochangia na kumpa fursa ya kupambana na ufisadi pamoja na usimamizi
wa Utawala Bora mambo yaliyopanua masuala ya Dedmokrasia Nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...