Maandalizi ya eneo la jukwa kuu ambalo watakaa viongozi
mbalimbali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa
zitakazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Jumapili.
Ujenzi wa kibanda maalum ambacho kitatumika kuwekwa mwili wa
Rais mstaafu Benjamin Mkapa kikiedelea kujengwa katika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam
Moja ya mafundi akiendele na ujenzi wa kibanda
kitakachotumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Baadhi
ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakiwa wamebeba choo cha kuhamisha
ambacho ni sehemu ya maandalizi yanayaoendelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam ambako shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa
zitafanyika kuanzia leo kesho Jumapili hadi Jumanne
Sehemu ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakijenga
hema kwa ajili ya maeneo ambayo yatatumika kwa shughuli mbalimbali wakati wa
kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakiendelea na kufunga
hema katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Moja uzio uliowekwa nje ya Uwanja Uhuru jijini Dar es Salaam
ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea siku ya kesho Jumapili ambako shughuli
za kunza kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zitafanyika.
Ujenzi wa kibanda cha kuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin
Mkapa ukiendelea katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kazi ya kuandaa eneo la jukwaa kuu ambalo viongozi wa
kitaifa watakaa ukiendelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa ngazi mbalimbali serikali pamoja na maofisa wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa kibanda
maalum ambacho kutatumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Baadhi ya mafunzi wakiwa wamebeba kikoo ambacho kikitawekwa
kwenye kibanda maalum kwa ajili ya kuwekwa mwili wa Rais mstaafu Benjamin
Mkapa.
Mabanda ya huduma ya kwanza yakiwa yamekamilika katika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shughuli ya kuaga mwili wa Rais
mstaafu Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(wa tatu kulia) akitoa maelezo
kwa viongozi mbalimbali wa Serikai kuhusu eneo ambalo mwili wa mzee wetu Rais
mstaafu Benjamin Mkapa utakavyowekwa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima zao za
mwisho zitakazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho
Jumapili.Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Seif Ali Idd.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanua jambo baada ya kufika
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya eneo
ambalo Rais mstaafu Benjamin Mkapa mwili wake utawekwa kwa ajili ya wananchi
kutoa heshima ya mwisho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi
Seif Ali Idd(katikati) akitoa ufafanuzi baada ya kutembelea Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya maandalizi kwa ajili
ya shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.Wengine
wanaomsikiliza ni viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Wazirii Mkuu Kassim
Majaliwa(kulia).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania(JWTZ) Jenerali Venancy Mabeyo akieleza jambo kwa Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa pamoja na viongozi wengine kuhusu namna ambavyo kibanda maalum ambacho
kitatumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kitakavyokaa kwa ajili
ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venancy Mabeyo
akiwa na maofisa wengine wa jeshi hilo wakielezekana jambo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Vijana,
Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa(wa pili kulia) na Makamu wa Pili wa Serikali wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar(wa tatu kushoto)baada ya kufika Uwanjwa Uhuru jijini Dar
es Salaam kuangalia maandalizi ya kitaifa kwa ajili ya shughuli za kuaga mwili
wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(katikati) akisisitiza jambo kwa
viongozi wa ngazi mbalimbali baada ya kufika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam ambako shughuli za maandalizi kwa ajili ya kuaga mwili wa Rais mstaafu
Benjamin Mkapa zikiendelea.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania(JWTZ) Jenerali Venancy Mabeyo akiangalia mchoro wa kibanda maalum ambavyo
kitakuwa baada ya kukamilika .Kibanda hicho ndicho kitakachokuwa na mwili wa
Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (aliyevaa suti)
akitoa maelekezo kwa maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
baada ya kufika Uwanja wa Uhuru kuangalia maendeleo ya maandalizi kwa ajili ya
shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Hassan Abbas(kulia)
akipata maelezo kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu shughuli za
kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambazo zinatarajia kuanza kesho
Jumapili ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam
kujitokeza uwanjani hapo kwa wingi ili kutoa heshima zao za mwisho kwa mzee
wetu.
Baadhi
ya waandaaji wa jukwaa kuu ambalo viongozi mbalimbali watakaa wakati wa
shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zitakazofanyika Uwanja
wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho(Jumapili),Jumatatu na Jumanne
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na viongozi
wengine wakijadiliana jambo walipokuwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(kulia) akiwa na viongozi wengine
wa Serikali wakishuka jukwaa kuu baada ya kufanyika kwa kikao ambacho kilikuwa
na lengo la kujadili mwenendo wa maandalizi yanayoendelea Uwanja wa Uhuru kwa
ajili ya shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiangalia jinsi
ujenzi wa kibanda maalum ambacho kitatumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu
Benjamin Mkapa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho.(PICHA ZOTE NA
SAIDI MWISHEHE-MICHUZI TV)
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
VIONGOZI mbalimbali wakiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Baloz Seif Ali
Idd na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wamefika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam kuangalia maendeleo ya maandalizi ya kitaifa ya eneo ambako
shughuli za kuaga mwili wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa zitafanyika.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
,Sera,Bunge,Vijaana, Kazi ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa
Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi.
Pia Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack
Kamwele, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sana'a na Michezo Dk.Hassan Abbas pamoja na maofisa wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama Venancy Mabeyo aliyeambatana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali
Yakubu Mohamedi.
Kwa kukumbusha tu mwili
wa mpendwa wetu,mzee Mkapa utaagwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
kuanzia kesho Jumapili, Jumatatu na Jumanne ambayo itakuwa ni siku ya kuaga
kitaifa ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria.
Akizungumza kuhusu maandalizi na hatua mbalimbali zinazoendelea hadi
jioni ya leo Julai 25,2020 ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ububakari Kunenge
amesema kwamba maanda
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kama ambavyo nimeeleza hapo
awali tutakuwa tunaendelea kuwahabarisha hatua mbalimbali ,hata hivyo kuanzia
saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi katika uwanja huo kutakuwa na Misa ya
kawaida na kisha wanananchi wataanza kutoa heshima zao za mwisho.
Pia amesema shughuli za kuaga zitaendelea na siku ya Jumanne
kutakuwa na ibada ambayo itafanyika Kanisa la St.Immaculate Upanga jijini Dar
es Salaam kuanzia saa moja mpaka saa saba.Hata hivyo ameomba ushiriki wa
wananchi kwa kufika kwa wingi kwa ajili ya kumuaga Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Hata hivyo amesema wananchi ambao watafika kwa ajili ya kuaga
mwili wa mzee Mkapa kutakuwa na maelekezo yatakayokuwa yakitolewa kwa ajili ya
kufanikisha shughuli hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...