Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

RAIS Dk. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi kwamba kuanzia sasa Uwanja wa Taifa utajulikana kwa jina la Uwanja wa Mkapa kama hatua ya kuenzi jitihada za Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika sekta ya michezo.

Dk. Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Julai 28,2020 wakati akitoa hotuba ya kumuelezea Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye leo ndio siku ya kumuaga kitaifa baada ya kufariki dunia Julai 23 mwaka huu saa tatu usiku jijini Dar es Salaam.

Wakati akielezea mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa wakati wa utumishi wake, alitumia nafasi hiyo kuzungumzia jitihada alizofanya katika kuimarisha sekta michezo nchini ambapo hata Uwanja mkubwa wa mpira wa miguu uliopewa jina la Uwanja wa Taifa ulijengwa.

Amesema baada ya kifo cha mzee Mkapa kumekuwepo na maombi mbalimbali ya wadau wa michezo na Watanzania wanaotaka uwanja wa mpira wa Taifa upewe jina la Mkapa,hivyo amekubaliana na maombi hayo.

"Mzee Mkapa alisimamia vema suala la michezo, sanaa na burudani.Uwanja wa mpira wa miguu unaofahamika Uwanja wa Taifa ni matokeo ya jitihada hizo, hata hivyo mzee Mkapa hakupenda sana vitu viitwe kwa jina lake. na kwa kuwa leo amelala usingizi najua hawezi kumuadhibu.

"Hivyo uwanja huu kuanzia sasa utaiwa Uwanja wa Mkapa au Mkapa Stadium kama sehemu ya sehemu ya kumuenzi kwa jitihada zake katika michezo.Mzee Mkapa alikuwa mwanamichezo mzuri na alikuwa shabiki wa Yanga.

"Ingawa hakuwahi kuniambia ingawa hata Rais mstaafu mzee Jakaya Kikwete amethibitisha hilo kwa kuwa na yeye ni Yanga, sijajua tu mzee Mwinyi yeye ni shabiki wa timu gani,"amesema Rais Magufuli wakati anazungumzia mchango wa mzee Mkapa katika sekta ya michezo.

Ameongeza kwamba hata COSOTA ambayo inahusika na haki za wasanii katika kunufaika na kazi zao ilianzishwa na mzee Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...