KAMPUNI
ya uzalishaji wa Mbegu bora zenye kuleta tija kwa wakulima Rijk Zwaan yenye
makao makuu yake Jijini Arusha imesema kuwa imejipanga kutoa elimu bora ya
kilimo cha Kisasa kwa wakazi wa kanda ya mashariki watakaofika katika maonyesho
ya Kilimo Maarufu kama nanenane Mkoani Morogoro.
Akizungumza
katika eneo la Vipando la kampuni hiyo Mjini Morogoro Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro
Naiman Molel amesema kuwa wakulima wa kanda hiyo watapata fursa ya kuelimika
juu ya mbegu bora za kilimo
Molel
amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa takriban miaka mitano katika
eneo hilo la nanenane na wamekuwa kwa kipindi chote hata baada ya maonyesho
hayo.
Ameongeza
kuwa hivi sasa watakuwa na mbegu mpya ya matikiti maji matamu ambayo yatakuwa
yakipekee katika maonyesho hayo ya nane nane kanda ya mashariki
Sanjari
na hayo ameeleza kuwa kampuni hiyo imendelea kutoa elimu kwa vikundi vya
wakulima muda wote katika eneo la nanenane pasina malipo
Ameongeza
kuwa hivi sasa wakulima pia wataelimishwa juu ya matumizi bora ya kitalu nyumba
(green House) ambapo wataweza kuzalisha katika eneo dogo
Hata
hivyo Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman Molel ametoa wito kwa
wakulima kufika katika banda hilo ili kuweza kuapata elimu zaidi
Maonyesho
ya Kilimo 88 kanda ya Mashariki ya mwaka 2020 yana kauli mbiu maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi chagua
viongozi bora huku yanahusisha mikoa ya Morogoro,Pwani,Tanga na Dar es salaam.
Vipando katika Banda la Rijk Zwaan Manyonyesho ya Kilimo Nanenane Mkoani Morogoro
Bwana Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman
Molel akionyesha nyanya zinazolishwa na kampuni hiyo.

Bwana
Shamba wa Rijk Zwan Mkoani Morogoro Naiman
Molel akiwa katika Kitalu nyumba (Green House) akielezea mazao
yaliyopandwa ndani yake ikiwemo matiki matamu (Sweet melon)
yanayozalishwa na kampuni hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...