Abiria wakisubiria mabasi yatoke kwenye kivuko ili waweze kupanda kuendelea na safari mara baada ya kushuka kutoka kwenya kivuko cha MV. Mwanza wakitokea upande wa Busisi wilayani Sengerema. Kivuko cha MV. Mwanza kinatoa huduma kati ya Kigongo wilayani Misungwi na Busisi wilayani Sengerema.
Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto na meneja wa TEMESA Mkoa wa Singida Mhandisi Awadhi Suluo  Wakikagua muendelezo wa ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ya karakana ya mkoa wa Singida wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo mwishoni mwa wiki hii.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWEN0 (TEMESA) 
Muonekano wa jengo jipya la kumpumzikia abiria wanaotumia kivuko cha MV. ILEMELA wakati wakisubiri kivuko, jengo hilo limejengwa upande wa Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza na tayari limeanza kutumika.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (wa pili) kushoto akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji Anderson Msumba kulia pamoja na meneja wa TEMESA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Margareth Mapela katikati wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya mji huo ambapo TEMESA Kahama imefanya usanifu wa mifumo ya umeme na inasimika umeme katika majengo hayo. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kushoto akiikagua ijnini ya kivuko cha MV. Misungwi ambayo ilikuwa ikifanyiwa matengenezo kinga katika karakana ya kivuko eneo la Kigongo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...